Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 31, 2012

NDOTO NDOTO


Nina kila sababu yakumshukuru Mungu ambaye anazidi kukuza kiwango changu cha imani siku hadi siku, kuamini hakuna kinachoshindikana kwakwe, haijalishi we ninani, una rangi gani, watu wametamka nini juu yako,uko kwenye ardhi ya nani, una umri gani haijalishi, umezungukwa na nani wala na nini haijalishi, kikubwa ni kwamba unaamini nini? na unawekaje ndoto ya maisha yako na kile unachoamini............

Kama mnakumbuka tarehe 26/08/12 nilitoa post ya Safari inaanza, ilikuwa ni tendo la imani ambalo ilikuwa kati yangu na Mungu.....ni siku niliyomwambia Mungu sasa yatosha! yatosha! yatosha! nimeona matendo yako mengi makubwa hili kwangu si dhani km utashindwa na km utashindwa basi itanipa woga mbeleni kwa kuamini  KWAKO HAKUNA KINACHOSHINDIKANA......nilimwambia Mungu huu mwaka usinipite nataka nikuoneeeee

Ndoto iliyonisumbua kwa zaidi ya miaka minne,miaka miwili ya kwanza nilijitia moyo siku ipo, nilifanya juhudi zangu zakibinadam nilijikuta nagonga mwamba, bahati mbaya sana nikajichanganya na jamii ambayo ilinifanya nione haupo uwezekano kabisa,na wengine walinijeruhi nakunicheka kwani walijua ndoto yangu,NIKAJIHAKIKISHIA MWENYEWE kwakuangalia ngozi yangu, hasa katika nchi ya ugeni, na pia niliangalia history za wanadam kwani, niasilimia chache sana ya watu walionje ya nchi kufanikisha ndoto yao ndani ya nchi ya ugeni.......miaka miwili mingine kabla ya tarehe 26/08/12 nilijikuta nimezima kabisa ndoto yangu yaani niliitandikia shuka nzuriiiii nakuilalia hahahahaaaaaaaa............Mtu pekee ambaye hakuchoka, kunitia moyo, hakuacha kuizungumzia ndoto yangu ni Mume wangu mpenzi, Baba wa watoto wangu,Mume aliyetoka kwa Mungu,ambaye aliamini pale nilipo si pangu, kuna wakati aliniona nimeridhika, kila nilipompa wazo la kubadili ndoto hakuniruhusu hata kidogo.....kila alipoingia na kupata nafasi yakuuliza ufumbuzi wa ndoto yangu hakusita na aliporudi nyumbani aliniambia,HONEY (in Slay's Voice) nimeongea na mtu fulani amesema tufanye 1,2,3....... hahahaaaa kuna wakati nilimuhurumia, niliona anahangaika bureeee haitawezekanaaaa.........AHSANTE MUNGU KWA KUNIPA HUYU MUME....
Siku moja kabla ya tarehe hapo juu nilijikuta nipo na positive people ambao waliniuliza maswali meeeengi ni kwa nini nimeizima ndoto yangu??? walinipa mifano mingi sana ikiwa pamoja na mifano yao jinsi walivyoweza fanikisha ndoto zao kwa kweli hawa watu walitumika kikamilifu kusema na mimi,Mungu awabariki sana sana na km mnanisoma wapenzi jueni kwamba yale masaa machache mliozungumza na mimi,Mungu anayakumbuka,mliokoa roho yangu bila nyinyi wenyewe kujijua........niliondoka na ujasiri mkubwa sana....
Tarehe 26/08/12 ni tarehe ambayo nilifanya maamuzi upya nakujichunguza mwenyewe nilifanya yote lakini sikujikubali kwamba pamoja na hatua zote nilizofanya nilisahau ukuu wa Bwana..............
Tarehe 31/10/2012 dakika 10 zilibadilisha kila kitu na kuona ukuu wa Bwana......ndoto yangu ilijibiwaaaaa, ukiniuliza ilikuwaje mi sijui jamani ni kwa neema tuuuuu.... kila kitu ni muujiza kwangu mpaka naandika leo bado nautafakari ukuu wa Bwana..........mwacheni aitwe Bwana na hakunaga km yeye na hatatokea


NILICHOJIFUNZA

1.TAMBUA NDOTO YAKO

2. USIIRUHUSU NDOTO YAKO IKAPOTEA

3.USIRUHUSU NEGATIVE PEOPLE WAKAINGILIA NDOTO YAKO

4.AMINI SIKU IPO YAKUKAMILISHA NDOTO YAKO

ANDIKO LAKUKUTIA NGUVU

Nayaweza yote katika yeye anitiae nguvu, hakuna linaloshindikana kwa Bwana, km bwana akisimama hakuna alie juu yetu,vita tulivyonavyo ni vya Bwana,tutaketishwa nawakuu,hatutakuwa mkia bali vichwa,tutainuliwa kutoka kiwango kimoja kwenda kingine

hahahaaaaa unatamani kujua ndoto yangu???????

Tuesday, October 30, 2012

WAWILI'S TYM


Nasikitika siruhusiwi kubeba Camera wala kupiga picha za wanangu........ningewaringishiaje ????? maana washakuwa chura kwa mda wa wiki mbili hasa huyo Careen hahahaaaaaa.....Mama mtu ukiniona nje ninavyotapatapa nahisi km wanazama mweeeee....mtoto sio muoga hata kidogo..... nilimuomba mwalimu niwachukue hapo tu.....kwingine nisingeweza coz kuna watu tofauti .Hizo ndo Sheria za nchi za watu, haturuhusiwi kuchukua picha bila idhini ya muhusika.......

baada ya swimming .............jamani eeeh kithungu sio lugha yangu hahahaaaaa maana najua kinanaiii lazima  wacomment  kwi kwi kwi




Sunday, October 28, 2012

TANZANIAN NIGHT


Mama wawili
Judy,I,Lilian & Sandra

Baba watoto.....
 frm right Jesca & huby,Olga,Mariam & Semeni
cute Semeni
Mariam,I & Jane
With Semeni's friend

Kaka langu na dada langu....Mustafa & dotie
girls mmetokelezea....... Mariam & Jesca
us
Ester,Mariam,Jesca& I



Mr & Mrs na zawadi ya best dress up mama hongera
with Judy & Isdora

With ney na dada letu
mimi penda weye girlfrnd
slay, Peter & Girls

Wanaumeeee....Slay with my shemejiz... Barick wa kwanza kushoto ndie mshind wa best dress up kwa upande wa wanaume Hongera my shemeji
girlfriend hiyo zawadi ulivyoing'ang'ania km yako!! hahahaaaaaa
my Girls

The End


Wednesday, October 24, 2012

OUT & ABOUT


Taking the girls to aswimming lessons
with my bby girl
muke na mama wa wawili
my best friends
jamani hakuna kitu naenjoy kuwa na wanangu mwee......though tunagombanaje sasa iwe cristabell kaniuzi  dada mtu will give me hug & kiss  atamwangalia mdogo mtu and say, Stop hurting my mum's feelings( in Careen's Voice) ,Cristabell  atakuja kunihug Mum am sorry.......so sweet....their r my truly friends...
my angels ( Sitaacha kumshuhudia Mungu wangu kwa ajiri ya uzao wa tumbo wangu) na kuwaombea sana wale wenye haja ya uzao.....Mungu ni Mwaminifu ipo siku amini hakuna alie Tasa....... mkumbuke Sarah kwenye Biblia  ndivyo Mungu atakavyokukumbuka na wewe...........

i love the place

with their teacher
nampenda mwalimu wao yaani anavyowafundisha kwa kuwabembeleza yaani hapa nilijifunza kitu jinsi yakudeal na mtoto ili aelewe kitu


washaanza kuwa samaki hapo kila corner yao
soon wataanza kunirusha roho mhehe mkinga mie na maji mwee utanihurumia
hahahaaaa hii picha kila nikiiona nacheka pekee yangu ilikuwa hivi......nilisahau mataulo yao nikaenda sehem wanayouza si nikajua bei zetu za kawaida duuu!!!!! nikashika hilo taulo bei yake sasa, nikapiga hesabu ya harakaharaka  akili ikaniambia hiyo ni kodi ya mtu vyumba viwili bongo na pia driving to my house ni km 5mins na mataulo yakumwaga..... hahahaaaa mkiga mie niliwavuta wanangu taratibu mpaka kwenye gari nikamtoa my bby girl nappy hao mpaka nyumbani.....

maskini hawana hata habari mumy kakimbia Taulo......
happy girls always
hatukupika jamani tulienda lunch with my friends from church
bbq chicken piza tamujeeeee
with makanaka( melody's bby)
with Lisa
Lisa,Rose & Melody

Lisa & Melody
us
two mothers & a mother to be........