MHARIRI wa Picha wa Kampuni ya Tanzania Standard Newspaper Limited (TSN), Athumani Hamisi ameziomba kampuni, taasisi, wizara na watu binafsi kumsaidia ili aendeshe maisha yake.
Kwa takribani miaka minne, Athumani amekuwa akitibiwa baada ya mwili wake kupooza kutokana na ajali ya gari iliyoharibu uti wa mgongo aliyoipata Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti, Pwani na kwenda kutibiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwenye Hospitali ya MilPark ya Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Athumani alisema kwa sasa amekuwa anatumia kati ya Sh 750, 000 mpaka 900,000 kwa mwezi kwa ajili ya gharama za chakula, vifaa na gharama ndogondogo za wanafunzi.
Alisema kila mwezi anawalipa muuguzi na msaidizi wake Sh 370,000 na ada ya watoto watatu ambayo ni Sh milioni 2.4 ikiwa ni Sh 200,000 kwa muhula mmoja kwa mtoto mmoja
KUSOM ZAIDI INGIA HUMU
jamani Mungu wa mbingu na nchi na azidi kumtia nguvu,,yani ajali za magari ni balaa kabisa unapata ulemavu pasipo kupanga wala kujua na wapo watu wengi sana wamepata ulemavu wa maisha kama uyu.hope anaendelea vizuri adi sasa na mkewe yuko pamoja nae
ReplyDelete