Pages

Ads 468x60px

Saturday, February 27, 2016

MAMA WAWILI.........


Na ubora wake


Vepe kwani?? ha!ha!ha! mnizoeagemaana na mimi nimeshajizoea sasakha!

ila msitu umekubali bwana duu!!!


Nawapendaga

Tuesday, February 23, 2016

NIPOGO.............

 Eti nani huyu, muuza chai wenuuuu...........mtajiju mwaka mpya na mambo mapya bwana ha!ha!ha!ha! mi nazidi kunoga tuu yaani......... ila sema hicho kifurushi huko kichwani nipo katikati niendelee nacho kwa kukikata kidogo au ndo niweke ka chemical just for a change....... 
kukenua vepe sasa ha!ha!ha!


msichoke bwana kuzurura nyie fanyeni km kijiwe chakurefresh ukikutana nacho haya usipokutana nacho nacho poa haa!ha!ha!

Nawapenda

Thursday, February 18, 2016

ONJA.............

Sio kwa ubusy huu........ Siku zinavyozidi kwenda bora ya jana aiseee ha!ha!ha! hasa kwenye masuala ya kublogua......... Ratiba yangu imekuwa tite kidogo.....  baada ya mabox hawa wanenu sasa wamekuwa aisee home work ninazozipata ni balaa......   natumia saa moja na nusu kuhakikisha tumemaliza wakati huo huo lazima nihakikishe wamekula na maandalizi ya asubuhi inayofuata.......   huku kwetu Bwana kila kitu kinakuangalia wewe. But am loving it aisee.......... na muda wa kulala nimegoma ile biashara yakumuacha Baba watoto wangu aende kulala eti mi napiga umbea bloguni mnikomeeeee nimegoma ha!ha!ha!  kwa $$$ ngapi mnazo nilipa???  Ha!ha!ha! hata kama natumikia wito unanafasi yake bwana.........asikwambie mtu kuanza safari ya usingizi pamoja na ubavu  ina raha yake bwana hasa baada ya maombi ya usiku km familia ha!ha!ha! (kitchen party hiyo). 

 Haya muonje hii basi mama Shughuli alialikwa shughulini ha!ha!ha! aka Bby shower



tuliita high tea wenyewe....

basi tuu fujo zetu ili kupendezesha siku ha!ha!ha!
 jamani hata niweke majina humu mnawafahamu??? nyie onjeni tuu ha!ha!ha!

 Jamani mlengwa huyo mwenye nyeupe bwana siakajifungua asubuhi wenzie tunajiandaa kumsherekea ha!ha!ha! akaona isiwe tabu mabest natoroka hospital nakuja  hata kwa masaa mawili ha!ha!ha! mi simo jamani  lakini siku ilienda ila mtoto alibaki na manesi hiyo ndo raha ya ulaya  mtajiju ha!ha!ha! inaitwa hapa kazi tuu



nawapenda nakuja kuzungumza soon ngoja nijipange

Wednesday, February 10, 2016

MAMA NA BINTI YAKE...............

kama ni urithi wakupenda picha baasiii Dada kubwa kashajichukulia ha!ha!ha!

Asione Camera hakupigi picha mpaka uanze nae .............

happy her.......

na Mama ake mwenyewe anasogea tuu kidoo ananifikia mabegani ha!ha!ha!
Usiombe unapiga picha huku unambembeleza anayekupiga picha majibu ndo hao sura haileweki unataka kuongea, umenuna ,au hahaha!


nawapenda

Monday, February 8, 2016

NIPOGO.........

Haya mniwone tbt zitaendelea mbele ya safari kama ikibidi ha!ha!ha!
sasa kabati la nguo, viatu begi lilihamia Tanzania ha!ha!ha! yaani  vilivyobaki ni sawa tuu naanza na moja   hii begi mtaliona sanaaa......

kununa vepe???


Muke ya Slay  huyoooo


Nawapenda

Tuesday, February 2, 2016

NYUMA YA PAZIA 2

Siniliwaambia tukaenda kijijiniiiii.......... Basi huko tulimfuata huyu bi mkubwa aliyemzaa Mama mkwe wangu, Kwa upande wangu hichi kizazi hakipo tena.........Hivyo tuliona kuna haja ya watoto kwenda wakaelewe na vile vile Mume wangu kalelewa na huyu Bibi wakati wazazi wamehamia kwenye miji yao.......... kwa kweli nilijifunza mengi mnoo hapa kijijini aisee, watoto walienjoy mnooo............. 
mzee anamaneno huyu hatari anakwambia vita vya Hitra  mi nilikuwa binti mkubwa sana..........(nyoo mi mnafikiri mi mwenzenu?? pumbavu zenu in her voice ha!ha!ha!).
ana mipasho ya hatari 

Anakwambia hao ndo mabest wake yaani usipomkuta kwake mtafute kwao ...........

Aisee jiko ndo nilikabidhiwa ha!ha!ha! nilikoka moto aisee, nilipuliza kuni ha!ha!ha! sio msosi wa watu wawili yaani ilikuwa ukitenga sufuria kama hakuna wageni basi idadi ndogo watu ishirini hivi kikikikiiii 


Team matembezi tulikuwa tunazunguka tuu kijijini huyo mtoto mdogo, mtoto wa mdogo wangu  watu walikuwa wanafikiri nae wangu ha!ha!ha!

spotted


Team no stress tulikuwa tunajizungukia tuu. Excuse nywele za Careen zilitakiwa ziwe za kubana alivyoona mwenzake bob basi akagoma kufunga......

 spotted

tukapelekwa shule aliyosoma Dad ake......ha!ha!ha! i wish mngesikia hayo maswali yaliyokuwa yanaulizwa na watoto wake kikikikiii!!
kuna picha moja Baba yao alipiga enzi hizo kwa pozi hilo la Careen na eneo hilo hilo , Sasa Baba yao anawakumbusha hiyo picha  basi ikawa kosa wakaanza kumtania eti na wao wanaiga pozi ha!ha!h!

my wawili my life!

 nimezipenda tuu picha nimeshindwa nitoe ipi niache ipi nikikumbuka namazungumzo ya hapo basiii!!


 Tukapelekwa na Darasani aisee wanangu wanahistoria kichwani........ Nafurahi kile nilichotegemea wakajifunze hapo kijijini walikipata na zaidi..........

Tunawapenda