Tulifika kihivi yaani??? kwa kweli ilikuwa surprise..... nature ya biashara yetu kweli inategemea upepo umekajee ... six days before ndo tukawa na uhakika wa safari hivyo hatukuweza kumshirikisha mtu mpaka nilivyokata ticket.....Ticket zenyewe ndo high season mkinga mie nilikuwa nahesabu mifuko ya cement tuu ha!ha!ha!........ila nilikuwa sina jinsi ha!ha!ha! so 5day before kufika Tanzania ndo tukaanza kuwambia wazazi watoke mikoani kuja kutupokea na wengine kuwasafarisha tukakutane kijijini zaidiiii ha!ha!ha!
ntakwambia kwa nini kijijini endelea kunichungulia...........nyie haya unafikiri kwa nini wenzetu wachaga tunasema wanaenda chimba dawa??? kuna baraka zake kuleeee. ila sema nene unafanyaje??? je inampa Mungu utukufu?? Ama ndo kuongeza maagano ???
kutana na watu wangu basi.......
Mama Rose mnamfahamu na Mama Suleiman je??? jaza nafasi zilizo wazi ha!ha!ha!
(yahaya unaishi wapi??? mbona unafikia mahotelini?? yahaya weee yahaya ha!ha!ha!ha!)
ngoja nijitetee jamani kibandani hatukuona hekima kusumbua watu wanaishi jamani kha!!!kwa mda wenyewe wa siku kadhaa............
na shangazi yao mwenyewe mimi namuita Mama mwenye nyumba . jamani huyo ndo Dada ake Mama wawili yaani toka yeye mimi nafuata........... ila kanidunda huyo utotoni kha!!!
Mutu na sheji yake tunamwita The Boss .......yee ndo bwana mipango yote ya mjini anatutoaje ushamba ha!ha!ha! Dogo tumekaa nae akiwa shule yaani ilikuwa kila kitu Dada Rose,Dada rose duu!! sa hizi nimerudi eti namwita boss wangu ha!ha!ha! (haya huyu ndo nilimuachia ziwa kwa Mama yangu...... kuoa Bado lakini ....wapendwa maono vepe??? ha!ha!ha!)
Boss hivi ile kesi ya makontena vepe imeisha ama?? Ha!ha!ha!
Bwana wee hivi mnajua Mama Rose mapenzi kwangu hamna kabisa habari yote iko hapa yaani.......
akisikia sauti tuu mbona atachinja ng'ombe!! ha!ha!ha! ila kwa Rose akijitahidi sana Kuku tena mgonjwa ha!ha!ha! joke jamani ila kuna kaukweli kidogooo
Eneo langu lakujidai mimi lipo hapa....... asikwambie mtu Bwana, sikilizeni hakuna eneo muhimu kama hili, Hili eneo linabaraka zake aisee,Tatizo lenu mnaingia fake mnataka kumaliza na uhalisia. Maeneo km haya ingia kiuhalisia, misingi yako isiyobadilika iweke sawa, ijulikane km black black, white white Kikubwa unyesha upendo wa kweli huku ukisimamia kweli...............Mwanzo inasumbua naweza kusema tena sana.........(ni kawaida hata paka anajihami akiona sura ngeni)....... ila ukikaa sawa sawa mbona system itakaa sawa........ yaani utadeka nakwambia..... mi mwenzenu hapa basi km ni mtoto mi mziwanda ha!ha!ha! kaka yenu atafuata badae.eee.....ha!ha!ha! Ila km uliingia Fake halafu unataka kuleta uhalisia wako mbeleni best hilo unalo endelea kuvumilia tuu ha!ha!ha! ndio maana ake si ulivumilia ili ndoa ikamilike basi tena, ndoa haishi mpaka kifo yaani tena ukicheza sana kuna baraka utajifungia....... otherwise omba Rehema ya ufunguzi kwao na utubu kwa nafasi yako.(wakubwa tuu ndo wanaelewa hapa na nyie watarajiwa kamata hii)
Kwa herini
Kwa herini