Pages

Ads 468x60px

Saturday, December 26, 2015

HELLO TANZANIA........

 Wapenzi huu ukimya  wa humu ndani wiki yangu ilikuwa busy sanaaa........... nilikuwa natakiwa nimeet mipango ya mabox kwanza  kabla sijaondoka so nguvu ilitakiwa iongezeke sana hii wiki akili yangu ilikuwa kihivi. Thank God tulimaliza ki hivi .........

last day @my workshop for 2015

kilichofuata ni safari Christmass yetu tuliifaidi Dubai. nilishindwa hata kuingia kuwa wish  ni matumaini yangu wote mlisherekea vizuri.
na mwisho kabisa naomba nipige hodi asubuhi nimeamkia nyumbani. Home sweet home jamani i love my coutry cha!!! nawaonea wivu aiseee. niko busy kubond ila ma bby seater wanabadilishana tuu na mimi na dad yake tuko busy kujihoney moon ha!ha!ha! nikubadilisha tuu viwanja ha!ha!ha!


 tunapokea mialiko ila bajeti yako kuanzia usafiri mpaka kulala ha!ha!ha!
 nawapenda

Thursday, December 17, 2015

BABA NA MAMA ...........

Tuiite TBT basi maana ilipigwa jumapili iliyopita ha!ha!ha! Tatizo muda wa kuingia humu aisee mpaka huwa natamani blog ndo iwe instagram or whatsapp maana huko huitaji ni moja kwa moja tukio tunaachia ha!ha!ha! haya basi mnifollow IG ili msiwe wamwisho kupata matukio mnaonja kule mkija huku  mnamaliza hamu am vepe............ @beyoublog ndo tunalotumia huko

Siku hizi bonding nyingi tunazifanyia kwenye maji aisee huku kwetu ni joto balaa ....... haya mtuone 

 naingia ingia siku hizi soon na mimi ntakuwa chura we ngoja ha!ha!ha!

Dah!! hebu tuangalie wenyewe ila kuna siku tukibadilikiana humu ndani utafikiri sio sisi ha!ha!ha!
mtajiju..................


 bukta vepeee ha!ha!ha! nyie mwenzenu bikini zimenishinda kabisa i must admit naona aibu aisee hasa kwa watoto .... yaani ikitokea wameingia chumbani kwangu wamenikuta na pichu watoto watatoka mbio km wameona sijui nini na am sorry mamii sasa huwa nawaza nikiwatokea nakabikini vepeee??? ha!ha!ha! ngoja kwanza niendelea kuwa mkulima kha!!

tunawapenda

Tuesday, December 15, 2015

MKONOOOO...

 Haha humu ndani dizaini km mnasahaulika  vile lakini nawapenda mnoo.... Sasa leo ,hii special kwa kijana wangu mkiingia huko chini kacomment sana sijui katokea wapi ???yaani halafu nimemiss ha!ha!ha1...... Kiufupi alikuja kupiga shule huku akakutana na Mama wawili  si nikamuweka mzigoni...... ha!ha!ha!ha1 tulipigaje mkono yaani .........maongezi yetu yalikuwa mkono baba mkono ushemeji baada ya kazi kikikikiii.... We jamaa nimekumiss umenifanya nikuletee hii post niliipost jana facebook hahahaa !!kaofisi ketu vepeee....... fanya kurudi huku niko na kijana wangu Kalist  bwana....... Stella  wa mgodini ahsante Mama kwakunitembelea huyo jamaa muongo fulani hivi amazing usimsikilize anayokwambia ha!ha!ha! joke joke.




 haya ntarudi wadau wangu maisha na bills duuu
  

Thursday, December 10, 2015

TUNAKUZA JAMANI......

Hii kwa kweli hata haikuwa yakupost...... ila nimeona nije nikutie moyo mpendwa ulie comment post iliyopita mamii.......

My dear  hii mbegu yenyewe iko hivi.......wee angalia  hao classmates wake nimepiga picha juzi walivyokuwa nakajisherehe kakumaliza darasa .......tofauti yao  hapo labda miezi tena kuna mwingine hapo same mwezi , mwingine kamzidi......... na hawa wengine ndo naona dizaini mbegu km mwanangu huyu mdogo ha!ha!ha!  so usione shida ni kawaida mnooo......We ni Mama bora bwana wee ........dont stress please .....

na huyo ndo aliyekuwa mwalimu wake wa Darasa .......na hilo ndo darasa atakalosomea Cristabell wangu mwakani ha!ha!ha! inaitwa bandika bandua aisee!!! chezea mapacha wewe???........ na uzee huooooo.......kikikiiii tufanyaje sasa???, nikukomaa tuu........ but am loving the journey aisee siku zinavyozidi kwenda ule umama na utoto naona km unapungua its more of BBF yaani naulizwa maswali yakikubwa tuu, najobolewaje sasa  na broken english yangu,????? nakosolewa na kusifiwaje???, yaani raha  tuu aisee..........Mungu aendelee kutupigania kwa kweli.

Habari nyingine hii  ha!ha!ha!


Bwana wee........ si nimekutana na  hii tena ,katika pita pita zangu duuuu!!! enzi zile yaani full kufuatana fuata yaani.... kusindikizana sasa duuu!! tulikuwa tunapenda kutembea khaaa!! hii kitu tulikatiza myfair pale ha!ha!ha!  nyie vijana wasiku hizi sidhani km photo point ya myfair mnaielewaaa ha!ha!ha!
kama sio miaka 9 basi 10 iliyopita  tulijiphoto point ha!ha!ha!

nimemwambia Baba wawili tukitia tuu timu bongo naomba kinyozi wake nimuone anirudishie hii look ya kijana wangu khaa!! na mimi mwenge  kwa wasusi itahusika aisee ha!ha!ha! ila sema nene Mama wawili sijui mkorogo au edit ilikubaleee ha!ha!ha! nikujisoap soap ilikuwa ha!ha!ha!

Nawapenda

Monday, December 7, 2015

MAMA NA TOTO KUBWA..............


Ukiwa na misele na wawili shurti bag kubwa na shughuli hizi za christmass basiiii bag full kujaa makololo
ananifundisha mapozi huyu mpaka concetration ya Camera huwa haipo ha!ha!ha!

ila nyie mwanenu kurefuka vepe....... 
hapo saba akifika kumi basi tena mdogo wangu ha!ha!ha! sema sura ndo zitaeleweka iliyokomaa itajulikana ya kikongwe labda nianze kutumia product za look young foreverha!ha!ha! zikigoma sasa kikikikiii

hili pozi letu ni lazima yaani....



ushamba vepe...

 tunawapenda