Pages

Ads 468x60px

Tuesday, June 30, 2015

YUPOGO......................

Nimepita tuu mwenzenu mabox yamechanganya mnooo............. ila nawapenda no mapicha mapya  hii nilipiga week ileeeeeeee ha!ha!ha!



akicheka ana pengo nani????

 akishangaa hana mapozi nani?




 akiringa sasa ha!ha!ha!ha!


Wednesday, June 24, 2015

MAMA WAWILI.......................


Chezea umodel wewe????

Mama ya nani huyu????

 blame on cameramtoto ana shida nyie acheni tuuu ha!ha!ha!



 excuse hayo maflaffy kwenye top ni huo mtandio mwisho wa siku nikajifunika sikujua km ndo uko na shida hivyo ha!ha!ha! uzuri imenikuta ndani ya gari shughuli ya siku ilikuwa imeisha ilibaki kuwapigia picha tuuu.......

Namaanisha kwa herini nanina wapendeni mnoooo......

Monday, June 22, 2015

TUZUNGUMZE.....................

Wapendwa naona haka kakipengele ka ndoa kila nilivyogeuza shingo last week nimekutana nako,  nimealikwa huko kwenye darasa la ndoa na mimi kufanya yangu, mara nikirudi kwenye darasa langu lakujisomea maandiko nikakuta na andiko fulani hivi ambalo nikajikuta nalishare huko facebook bila kujielewa why nalishare.



 kizungu kikigoma kajisomee mwenyewe mithali 18:12 ha!ha!ha!ha!  tuendeleee.......

Leo  asubuhi nimeingia kwenye  facebook page moja nikakutana na hii topic ambayo imeletwa kutoka jamii  forum kama ilivyo . huu ujumbe pia ukawa km unachangia changia nakunisukuma niseme kitu...

 Jisomee mwenyewe

Mimi ni mwenyeji humu ndani ila tu kutokana uzito wa habari hii niliona nije under cover kwa miaka 4 niliyokaa Jf kuna ambao tunajuana personally na ni wengi tu.
Ndoa yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.
Hatukuwasiliana tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika pale nyumbani.
Tukapeana jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."
Hivyo nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.
Tukiwa kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo. Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama mkwe aliogopa kuzitazama.
Saa kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la hubby.
Tulipofika tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka asubuhi na mapema.
Anyway, kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.
Wamepandishwa kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea, sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.
Tulikotoka na mwanamke huyu:-
Kiukweli Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe, amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11 jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)
Wakuu, mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.
Akienda kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa hajawahi Ku cheat.
Simu zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaño yote na wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.
Sababu niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.
Hati zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.
Maana nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea. Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau, tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana. Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa wanaona I am not acting like one.
Mungu akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.
Nikamjibu mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile anamwangalia shetani.
Anyway nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri, nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine atabadilika.


kiukweli mi sio mchangiaji sana huko kwenye magroup napitaga tuu ila huwa najifunza mengi.Nashukuru Mungu maadmin huwa wananipotezea ikifika muda wa fagio ha!ha!ha! nimepona kwingi  ha!ha!ha!ha! sijui ni uvivu au huwa naona sio kila kitu na mimi niseme hata sijui lakini hili kuna ule moto ndani  yangu ambao sikuweza kujizuia kupita bila kusema neno nilisema hivi,.......


Endelea chini kabisa kwenye alama nyekundu


Nimejikuta napata moto tena kulileta huku ambako naweza kuongeza nyama nyama zakitumishi ha!ha!ha!

  Wapendwa tuelewane tunaposema unconditional love limebeba pande zote mbili, inategemeana na juhudi zote za pande zote .Wapenda hata Yesu alikuja kuokomboa ulimwengu eti eeh!!! lakini je kila mtu atauona ufalme wa mbingu????   jibu ni no..... why kwasababu kuna nafasi yako yakuikamilisha hiyo inaeleweka.Sasa basi,
  nielewavyo mimi huyo Kaka hapo juu tatizo sio kubakwa  kama sio shida za bidada  (siwezi kusema mapungufu maana mapungufu huwa tunasaidiwa na roho mtakatifu na hata waume/wake zetu km tukijitambua) uamuzi umebeba uchafu mwingi ambao in either way upande wa pili umeshindwa kuwajibika.

 Rejea kwenye hilo andiko la mithali 
"kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna"  Kile kitendo cha mume kukuuliza mbona umefanya bila kunishirikisha wewe ukajibu ndo ishakuwa......... hilo jibu limejaa majivuno na jeuri ndani yake nielewe (imewahi kunitokea  huwa kunakuwa na karoho fulani mda huo kuna mtu atanielewa lakini baada ya kujitambua kuna kitu unatakiwa ukifanye bwana eeeh!!!  na hakitokei mara kwa mara ikiwezekana hakirudii tena otherwise una shida)

 Bado hainikai vizuri kweli wanawake tunamikakati yakujikomboa lakini bado haitabadilisha nafasi ya uke. Sipati picha umeamka asubuhi unamwambia na somewhere kukutana na madalali ha!ha!ha! nacheka because nimekutana nao sana hawa watu km Mume wangu hakuwepo nilihakikisha nina kijana pembeni no matter what awe mdogo wangu au shemeji yangu Sasa najiuliza ule ujasiri yakujiandaa nakuaga  duuu!!! jamani kweli hiyo ndoa baridi Mwanaume hata kale kajiwivu basi kusema nisubiri nikusindikize kwa hiyo mibaba, basi hata kusema mkutano utakuwa wapi just in case? au hata kusema nipigie simu mapema nijue umnaendeleaje japo kuwa sio deal inayomuhusu ile tuu kumjulia mkewe yuko safe.............. Najiuliza tena nimeshindwa kumuomba Baba watoto anisindikize very Friendly bwana mwenzio nina nina famili business somewhere hebu nipe company  na vitu km hivyo na hapo ndipo tunamalizia andiko "Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu".. umeogopa asijue nini sasa?  asiwajue hao watu unaenda kuonana nao?? naona kama kichekesho umefanikiwa ficha hati zako za familia yenu ambazo ziko kwenye jina lako mwanaume hata hashughuliki nazo kutaka uzione kitu kinachonithibitishia kwamba hana shida na mali zako, unaenda kwenye hayo madeal unamuaga unaenda na anakuruhusu kitu kinachonithitishia ana kupa uhuru wakufanya mambo yako  waulize wanawake wote km hawata kwambia how blessed you are........ila unaficha madeal yako sehemu gani yatafanyika kweli???......... haya sasa yametukata yakutukuta guess what?? saa tisa usiku ndo muda ambao hujawahi kupitiliza pale ndo alipoona kwa kunaweza kuwa something serious kimekupata........ Yes bado anakujali mnooo!!! you're trully  blessed!!!

 Nimesoma comments na wengine wanasema sijui labda kabla ya mambo angemuitia watu sijui mara mama mkwe sijui ndo tatizo ... ngoja niwambia mimi huwa naamini ndoa yangu ni yangu , naheshimu mawazo ya watu lakini huwa naamini  mziki wa ndoa wyangu wakuucheza ni watu wawili. nimeshuhudia sana hizi ndoa za vikao mwisho wa siku huwa zinakatika gafla. Mama yangu  huwa anaamni  Mume niliyenae hajawahi kumuona kwenye ulimwengu wake tangu azaliwe, humwambii kitu yaani hata ikitokea amedokezewa kitu na mtu atakwambia mimi ndio tatizo guess what ?? ndani ya miaka 7 iliyopita kunawakati niliwahi kutaka kukusanya vilago ha!ha!ha! no body knew...... naniliamini kabisa hakuna ambaye angeweza kunielewa maana kila mtu asingeweza kuamini just because sisi sio watu wakujisema sema na tunamshukuru Mungu ametupa ufahamu wakutambua mapungufu yetu na kubebana kile kilikuwa ni kipindi tuu chakutambuana.  na pia hutukutu tunavyo move on tunamove namabegi ya uchungu mioyoni mwetu we make sure  tuko sawa tunazungumza sana so whatever we display kwa sasa is real ha!ha!ha! likitokea lakutokea ole wenu niwasikie he situlisema sisi walikuwa wanatutumia mapicha wako happy kumbe wanaigiza tuu ha!ha!ha! mshindwe manabii wa namna hii.kha!.......... but again am not saying we are perfectooooooo. ha!ha!ha!

 ninachotaka kusema Mama anabaki kuwa Mama inapofikia tunabusiness na Mama mume wangu anaweza juu juu (inategemea) japo hata kuwa na maamuzi labda ushauri. Na inapofika kwenye mambo yangu na Mume wangu familia yangu wanalijua hilo hawana nafasi. kwanza wameshaambizana huko na mara nyingine utasikia ndugu yetu tunaomba basi hili Mumewe asijue ha!ha!ha! huwa nawambia i dont promise you ila akijua halitakuwa km mnavyolijua nyie atakuwa tuu aware just in case. why kwa sababu unataka kuweka misingi mizuri ya mahusiano pande zote mbili ili kuwe kuna heshima na kuthaminiana.

JAMANI JAMANI SIJASEMA NIMEFURAHIA LILILOMKUTA MWENZETU ILA TUMEJIFUNZA NINI KUPITIA MWENZETU.

 Nimemaliza ha!ha!ha!



 

Monday, June 15, 2015

NIMEKABWA...............

Nyie bwana mwenzenu nimekabwa yaani................ kuna hii sheria imepitishwa karibu nchi nyingi huku kwetu bado ila ndo ishawekwa kwenye mazungumzo... kwa jinsi gani inavyonikaba yaani natamani nipewe kipaza sauti niongee, niende koteee linakozungumziwa kulipinga jeuri sina yaani nikama  kasisimizi ntakavyoonekanaha!ha!ha!ha! Sasa tatizo hata huku uchochoroni ninakoweza kusema aiseee kiinglish mgogoro yaani kinapoteza ujasiri wooote..... nakasirikaje sasa!!! ha!ha!ha!

 Jamani hiki kitu kinachooitwa jinsia moja wandugu ni laaana, yaani laana hii kitu............... km hamuelewe ndo ilimaliza Sodoma na gomola Someni MWANZO 19 , Mambo ya walawi 18:22,20:13 unajua inaogopesha sana ... jamani acheni dhambi iendelee lakini kuipitisha ionekane ni kawaida jamani uuuwiii!!! kweli Damu ya Yesu itufunike... Vizazi vyetu hivi maana sasa mpaka mashuleni itaingia huko ndo wanenu wanashinda, ikishakuwa Sheria na makanisani nayo itapiga hodi tuu  yaani kweli shetani katukalia uwiiiiHasira ya Mungu haita tuaacha aisee................Duuu!!! mwenzenu wiki iliyopita nahisi nilikufa ganzi kabisa  naona nimeanza kurecover....Yaani hofu ya Mungu hatuna kabisa yaani mi sijui sijui sijui

 tuendeleee na mapicha tupotezee mawazo kidogo khaaa!!!

Eti huyu nani???



 nimewarushia huko hii picha nimewambia the face you make mtu anavyojitahidi kukushawishi anaamini neno la Mungu lakini kunavitu tunatakiwa kuvifanya kwa sababu ya vile aonevyo yeye vinamfaa na kuvihalalisha kukufanya na wewe uone kawaida aiseee shetani ana mbinu nyingi nyie.... to me huyu mtu haamini neno la Mungu bali anajiamini yeye mwenyewe kuna roho inatumika hapo nyuma ya mtu aisee.......... Unajua nini sisi sote hatujakamilika lakini yale mapungufu yetu tujitahidi yawe yetu why kutaka kumshirikisha na mwengine aone kawaida??? kumbuka kuna wengine ni wachanga unapokuja wewe ambaye tayari unajua kweli lakini unaificha kwa huyu mchanga unategemea nini???


haya mbarikiwe ila ndugu sugua goti maana hatariiiiii

Tuesday, June 9, 2015

MAMA WAWILI......................

Ila nyie mwezenu leo Bwana kanitendea tena............ yaani hilo tabasamu hapo mnaloliona  kwa shetani kimenukaaa.........Kagalagazwa chaliiiii....Chezea Kibari cha Mungu wewe????!!!!  
Hamuambiwi  ila mnachotakiwa kujua Unachoona hakiwezekani kwako kwa  Mungu is just a dot yaani......... tena unajua nini???? pale akili yako inapochoka kabisa hata kujiongeza haiwezi pale ndipo Bwana anapojitwalia utukufu................... Nimemaliza siendelei ng'o .....................maana shetani alivyokipofu naanzaje sasa kumponya??? hafai hafai akafie huko wana wa Mungu tupiteeeeee.

Haya mapicha time
jamani eeh kwa ajili ya watoto wenu nimeamua kufuga nywele kidogo naona umekuwa wimbo sasa mara nyingi wananiambia Mumy why your hair looks like a Boy???  you should do like............. or put a wig (in CareenVoice)  Majangazi............sasa ngoja tuwafurahishe eti eeh?? ha!ha!ha! Ila ndo bado sijajua natokaje Kikikiii ujue ukitoka kwenye hizi style jamani kurudi kwenye manywele sijui unajionaje......... nimejifungia ndani kujivalisha mawigi khaaa!!! najiogopa ha!ha!ha! anyway let see

Halafu mi nawadanganya mjue jeuri yakwenda nilikoenda na hiyo yakuangaza niliitoa wapi??? Ki!ki!ki! Sweta hiyo mkononi ilihusika ........ila  nyie wapenda mapicha ndo nimewakomesha Ha!ha!ha!



Friday, June 5, 2015

ONJA................

He wandugu hii wiki mbona imekimbia hivi??? kha!! binafsi hata sijaielewa kabisa ha!ha!ha! kwanza humu ndani niliwasahau kabisa yaani  mwee.............. haya onjeni hizi.... si niliwambia nilikuwa nakajievent halafu kale kapepo kakanifanya nisibebe Camera shughulini  ha!ha!ha!ha! haya hizi nimefanya  kurushiwa tuu nawalioweza kutuspot ha!ha!ha!   ila baadae nilijilaumu aisee maamuzi hayakuwa mazuri kwa mpenda picha kutokubeba Camera  kwenye tukio km hili kweli nilijikosea  aiseee anyway..............

B&us


Shoga yake, Dada yake mie nae akajiongeza........

na warembo wangu..........

 Tumenyooka  hapana chezea ha!ha!ha!mpendwa hatua zilikua kubwa aisee sinikachana gauni ha!ha!ha! (joke)

Boys  nao walikuwepo aisee si mchezo Camera tuu ndo haikuwatendea haki lakini duuu!!!

 Haya basi muwe na weekend njema