Ndugu zangu wapenzi?Watanzania wenzangu ni maombi yetu sisi tuliokaribu na Marehemu. Tunaomba mtusaidie hizo picha zisitumike hasa za mke na watoto kwani hazihusiki na wala tunaona hakuna sababu ya leo kuwajua mke au watoto kwa namna hii inayosambazwa km hamkuweza kuwajua kipindi muhusika yuko hai.
Ukituuliza bila kutuonyesha huo ushahidi kwa kweli tusingewaelewa, lakini tunashindwa na mtu pekee wakutupa majibu ni yeye ambaye hata sasa hasemi jamani wala haoni, yuko kwenye barafu ameganda hata tukamtikise vipi haiwezekani..........kilichobaki ni kumpa heshima ya mwisho. Kwetu sisi bado tunaamini alikuwa ni Baba aliyewajibika na kuwapenda watoto wake, alikuwa ni Mume aliyempenda sana mke wake japokuwa ana hayo mapungufu ambayo tumeweza kuyasikia kama yanavyosambazwa, na pia alikuwa ni rafiki mwema sana,sana sana. Kuna mengi yaliyojificha ambayo hamyajui na tunayaheshimu sana ambayo tusingeweza kuruhusu akili zetu zitawale na hizi habari ambazo sio nzuri badala yake tuendelee kuomboleza nakumuombea kwa namna na jinsi alivyokuwa wa thamani kwetu.
Hata kama alifanya hivyo ndugu zangu watu wake wakaribu tunaamini alifanya kwa usiri maana hatukuona tofauti yoyote ya uwajibikaji wake hivyo kwetu ni heshima kubwa mnoo hayo mengine ni yeye na Mungu wake.
Tunaomba mtusaidie hili ndugu zangu binafsi nimeshindwa nimejitahidi kukimbia social media na hata sikutegemea kupost lakini bahati mbaya sasa kwa sababu zisizozuilika unajikuta umeingia na kukutana na haya....... ndugu zangu inaumiza mnooo hasa unapoona mke na watoto wananyooshiwa vidole..........wapenzi Jamani mbona hakuwa that much evil jamani..........
Tunaomba ndugu zangu tunaelewa tayari imeshakuwa lakini mnaweza kutusaidia kupunguza hii speed yakuenea na kutokuifanya aonekane kama hakuwa na utu tena. mkishindwa kabisa basi mturuhusu tuwe kwenye hali ya utulivu hadi hapo atakapoingia kwenye nyumba yake ya milele.
Ahsanteni
Gone to soon Lusekelo jamani RIP.