Hivi Ze kupendana day ndo kesho?? Ha!ha!ha! Halafu eti nasikia mmeweka mgomo........Mapenzi sio kupendana tena imekuwa mambo $$$$
Ha!ha!ha! ila bongo mnatisha mjue????aisee hivi mnajua mnavyotutoa stress za mabox tukiingia huku mitandaoni?? Duu kweli home is a sweet home yaani...........
anyway back to the topic
Nimejikuta nimewaza sana kwa habari ya wakati, kuna maneno mengi huwa siyaelewi wala kunikaa. Sijui kwako mpendwa unalipokeaje..... Binafsi naona kama kifungo........
Nanukuu.....
14 Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
15 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.
16 Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
17 Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
Majaribu ni pito ambalo kila mwanadamu hupitia, Hatuzuiliwi kufurahia leo eti kwa kuhofia muda wangu wajaribu ukifika ntaiambiaje jamii???Tulio wengi tumejikuta mtu akijaribiwa tunamuhukumu kwa ile furaha yake aliyoonyesha kabla ya jaribu kumkuta..... mfano mtu kajiselfie anavyokula bata na mumewe baada ya mda fulani shetani kapita kwenye hiyo ndoa Duuu!! wenyewe(Kifungo) utawasikia sialikuwa anaringa na ndoa yake............ sialikuwa anajifanya yeye ndo............. nimetumia ndoa kama mfano kuna maeneo mengi ya maisha km umelengwa kunielewa utanielewa.
Sikia nikwambie, Hivi unajua Shuhuda za kweli zinampa Mungu utukufu?? Tatizo sio aliyejaribiwa ,Tatizo unalo wewe unaetoa maneno ya dizaini hiyo unashindwa kutofautisha wakati.Na unashindwa kutambua watu tunatofautiana jinsi yakuyaweka mambo .....
Ni kweli tunahitaji hekima maana unapotoa ushuhuda unatangaza vita na shetani, lakini mpendwa kwani furaha yako yakuigiza au ni kweli inatoka kwa Bwana??
Mkumbuke Daudi alicheza mpaka nguo kuanguka kwa sababu amebeba utukufu wa Bwana, Tumemuona Mungu akimtetea mnoo........na Pia huyo huyo Daudi tunamuona akiomboleza mara baada yakuletewa ujumbe na Nathani nakutambua makosa yake na hata mwanae alipokufa alinyanyuka kula na kwenda nyumbani mwa Bwana kuabudu.
Jiulize,
Unafikiri kwa nini Yesu alisema Siku zitakuja watakapoondolewa Bwana harusi ndipo watafunga??? Nidhahili kuwa Duniani tumejaa mchanganyo Shetani kila kona anatuwinda, tunajikuta tumemfungulia mlango kabla hutujajielewa majanga yameshatokea Kako fasta mnooo.......... Muulize Daudi kilichomfanya aache kwenda vitani apande gorofani ni nini?? acha na hiyo kilichomfanya amkodolee macho mke wa mtu badala yakukimbia kuona alichokiona nini??
Kuna siku ntakuja humu kuwaa,bia kuna jaribu moja nilipitia km miaka 5-6 iliyopita nilivyokuja kumjoin my Baba watoto.. Aisee Kama sio neema na hekima ya Mungu jinsi nilivyodeal na hiyo situation leo naangalia nyuma na muona shetani tuu alishikwa na aibu...........
Mwisho wa siku utakubaliana na mimi jaribu ni namna unavyodeal nalo kikubwa nikuomba neema ya Mungu lakini hatujimi kuenjoy ile furaha uliyonayo kwa kumuogopa mjaribu........ narudia tena hicho ni kifungo cha kutokuwa na moyo wa shukrani mbele za Mungu,Kutokuridhika na kile ulichobarikwa kwa sasa, na pia huna uhakika na unachokiamini au kukimiliki...... Unafikiri Kwa nini Daudi bado alinyanyuka kufuta machozi,kuoga na kula akamalizia kwenda kumwabudu Mungu maana alijua anayemwamini.............
Haya ngoja nimalize na kesho ndo ma full show off ya Valentine jamani muwaache....... let them be..... we km unagulia sugua goti Mungu akuvushe kwenye huo mjaribu kuliko kutetemeka kwa hasira za chuki nyuma ya komputa, unajua nini unaongeza donda ha!ha!ha!ha!
As for mama wawili here no mashauzi mwee ........ Baba watoto anapiga mabox ya usiku akirudi ni full kulala ready for another night kwi!kwi!kwi chezea shift??? Jamani si tumesema wenyewe tunataka $$$ no maua na kadi??? haya sasa ndo kulazwa mzungu wa nne zikatafutwe hizo $$$ uletewe Kwi!kwi!kwi!
Ndugu zangu wa insta nyie mnitag tuu sina shida mnidobolishe mashauzi ha!ha!ha!
love you..........