Pages

Ads 468x60px

Friday, January 16, 2015

TAFAKARI..........................

Jamani leo niko kiupako zaidi ha!ha!ha! sijui kwa nini, hili neno nimekutana nalo kama wiki iliyopita kwenye muda wangu wakujisomea Biblia, lakini nimejikuta  mpaka sasa halinitoki nalitafakari , nalichambua,..........,....... duuu!!! mpaka nimeona labda yanipasa kukushirikisha na wewe......

Linapatika kwenye kitabu cha Luka 7


Baada ya Yesu kumaliza kusema haya
yote watu wakiwa wanamsikiliza, akaingia
Kapernaumu. 2Mtumishi wa jemadari mmoja wa
Kirumi, ambaye bwana wake alimthamini sana,
alikuwa mgonjwa sana karibu ya kufa.

 Nilitafakari kwa habari ya, 

Mahusiano kati ya hawa wawili nikajipa moyo inawezekana hata kama kwangu mwenyewe haijatokea basi nimeona kwa macho haya mahusiano  yaani nikimaanisha sio tu tunamabosi wazuri wa dizaini hii pia nimeshuhudia hata mahusiano haya kwa aliyekuwa nacho na asiyekuwa nacho.  Nafasi za watu hazikwezi kiasi kwamba zikapoteza ubinadamu. (Japo  bado tunahitaji wengi wa hivi)

nikaendelea mbele

3Jemadari huyo aliposikia habari za Yesu,
aliwatuma wazee wa Kiyahudi Kwake,
wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo
jemadari. 4Wale wazee walipofika kwa Yesu,
wakamsihi sana amsaidie yule jemadari
wakisema, “Mtu huyu anastahili Wewe umfanyie
jambo hili, 5kwa sababu analipenda taifa letu
tena ametujengea sinagogi.” 6Hivyo Yesu
akaongozana nao,

 Nikajiuliza  kwanini amewatuma wazee???
Nikajipa majibu mwenyewe kwa tafsiri yangu  mara nyingi kwa mzee tunapata busara, hekima, na zaidi chumvi nyingi ha!ha!ha!
Hapo ndipo nilipoanza tafakari nyingine, je ????nimezunguka  na watu wa type gani?heshima yangu na thamani yangu imebebwa na watu gani? Je wamesimama na mimi? wanatambua mchango wangu ???japo mimi ni binadamu namapungufu yangu  je??? nikipi wanachokiona zaidi je nimapungufu au  kile kizuri???

Haya mdau wangu na wewe tafakari hii.......

 Duu!!! nikaendelea kidogo hapa ndipo paliponipa mawazo mnooo!!1 

 lakini alipokuwa hayuko mbali na nyumbani,
yule jemadari akatuma rafiki zake kumwambia
Yesu, “Bwana, usijisumbue kwani mimi sistahili
Wewe kuingia chini ya dari yangu. 7Ndiyo
maana sikujiona ninastahili hata kuja kwako.
Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu
atapona. 8Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu
niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari
chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye
huenda na huyu, ‘Njoo,’ yeye huja.
Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hili,’ yeye
hufanya.”
Ngoja niwambie aisee.... humu ndani mwangu nina kajisebure huwa sikatumii sana,ni theater room kwa wale mtakaonielewa huwa nakatreat kidizaini fulani hivi special ha!ha!ha! hao wanenu wenyewe wakiingia wanakaa kwa adabu wanajua no messy otherwise mumy will be mad!! Sasa kwa sababu kichwani mwangu huwa naimagine kumualika mtumishi fulani mkubwa huko ha!ha!ha! yaani huwa napata picha na yeye amekaa  humo na mimi,ki!ki1ki!  Shemeji yangu naye mmoja aliwahi nitembelea akaniambia yaani shem!! duu unafikiri ukimualika Mh.K humu ndani atakubali kwenda kulala hotelini yaani atakaa hapa(in his voice)huku ananionyesha pozi atalokaa Ha!ha!ha!ha! ( mcheshi fulani halafu mwanasiasi basi wee)

Haya hizo porojo nataka nikulete huku niliendelea kutafakari kama ningekuwa mimi aiseee!!! zile ndoto sijui za mtumishi sijui Raisi hapo ndo ningejipindaje Yesu anakuja!!!! weee ningeita wapishi, wafanya usafi nahisi ningewalipa 24hrs,yaani ni full kujitanua na kile nilicho nauwezo nacho,  hiyo yote kumfanya Yesu afurahi.....Mpumbavu mimi bila kujua he is more than that, na mara nyingine hiyo nafasi inaweza kunikosesha, Vipi kama nisingejaliwa hivyo vyote?? Je nisingemkaribisha??? na kwa kusema hivi sijasema unapofikia kwenye suala la ufalme wa Mungu basi tusitumie mali zetu na vitu kama hivyo .......... Nenda kamsome mwanamke aliyempaka Yesu mafuta yathamani alipokuwa anakaribia kwenda kuteswa, watu walimshangaa?? Yesu aliwajibu nini???

Ninachotaka kusema ni kwamba inapofikia kwenye ufalme wa mbingu kuna vitu vinaambatana navyo,  kuna haja yakuomba neema ya Mungu ujue unakabiliana vipi, na hii pia ipo kwenye maombi, Kuna haja yakujua nafasi yako kama muuombaji iwaje???  Sikumbuki nikitabu gani ila kuna yule aliyesogea mbele za Bwana nakujinadi, oooh! mimi nimekufanyia hivi na vile, sijui nimetoa sadaka, nini na nini . na mwingine alichoweza nikujipigapiga nakukiri yeye ni mdhambi....(Wasomaji mnanielewa) hivi unafikiri huyu aliyekiri kuwa yeye ni mdhambi hakuwa na hata moja zuri ambalo angeweza kumwambia Mungu hata mimi nilikufanyia hili????

Tafakari!!!!


9Yesu aliposikia maneno haya alimshangaa
sana, akaugeukia ule umati wa watu uliokuwa
unamfuata, akawaambia, “Sijaona imani kubwa
namna hii hata katika Israeli.” 10Nao wale watu
waliokuwa wametumwa kwa Yesu waliporudi
nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona.

Halafu unajua nini hayo yote alituma hakutaka kujitia kimbelele aonekane, mara sijui nini duuuu!!!! na muujiza wake akapata.

 kwa kweli nimeguswa na kila kitu hapa kuanzia ilivyoanza mpaka uponyaji ulipotendeka aisee!! nilijikuta mpaka chozi limenitoka na kikubwa nimejifunza kitu.......

 Haya mwenzangu uko wapi? nafasi yako iko wapi?


POLENI KWA GAZETI KAMA VIPI NISIPOST NEXT WEEK YOTE ILI MPATE MUDA WAKULISOMA ha!ha!ha!

No comments:

Post a Comment