Pages

Ads 468x60px

Tuesday, December 30, 2014

LATE POST..........

Jamani siku zinakimbia duuu!!! sitaki kuamini tumebakiza masaa eti????? Kwa kweli ni kwa neema!!!!

 Haya naona matukio mengine yatakuwa so 2014 tuyapotezee tuu ngoja tulimalizie hili......... Sasa basi wenzenu sijui ndo ushamba au ndo sio watu wakujipanga hata hatujielewi.... Tulikuwa tuna sehemu kadhaa ambazo tulijisemea Mungu akitujalia tutaenda kusherekea Christmas huko .... so hata mialiko tuliyokuwa tunaipata miezi miwili kabla ya wenzetu ambao huwa wanataka kujua nani mgeni atakuwepo ilibidi tuwambie hatuta kuwepo...........

 Tukaendelea na mabox kama kawa, wiki mbili kabla ndo tukaanza kujua ni wapi kati ya kule tulikotegemea kwenda  na tuna uwezo nako maana sehemu ni nyingi  mshiko nao lazima uhusike ha!ha!ha!ha! so kabajeti kakawa kanaruhusu sehemu fulani .... heee ile kupiga simu ni full kujaa tena unaambia till next year duuu!!!!

 Isiwe shida!!! tukaona tutajiachia humu humu ndani kwetu ila kivipi??? Ha!ha!ha! ile mialiko ya too late tukaanza kuipokea sasa wee ilituwekaje busy??? sasa kuna Mualiko mmoja tulikuja kubebwa kwenye basi kwenda kuzunguka  kuangalia watu wlivyopamba nyumba zao Christmas lights duuu!!! nyie kuna watu wanajua kusherekea aiseee!!!! 

Hapo ndo makelele yalipoanza ndani mwangu........... Mum&Dad why dont we have a christmas tree in our house??? ni why?why?why? mpaka mzazi unaanza kujistukia ha!ha!ha!Hapo ndo tulipopata idea  nini chakuwafanyia ili wajione hata nyumbani kwao kulikuwa na christmas.

So siku mbili kabla ya christmas nikaenda nao duka moja tuu ambalo nilijua ntapata kila kila kitu watakavyopenda, nikawambia lets make a list just incase Santa anakuja nyumbani kwetu tumuombe atununulie nini.......... Walichaguaje sasa hivyo vikololo?? nikabahatika kupata na haka kacheap Christmas tree .............. hao Tukarudi zetu nyumbani.

Shughuli kesho yake Mama mtu nikaenda kuvinunua nikarudi kuvificha. Siku ya christmas tumerudi tulikotoka usiku mweee !!! ikabidi tuwambie guys mnatakiwa mkalale saa hizi, ili tuwahi kuamka kesho ndo Siku ya Santa kuja (BOXING DAY) Ha!ha!ha! 

Shughuli ndo tulikuwa nayo sasa na Baba mtu tumekesha kufunga hivyo vizawadi, kuja kustuka  saa nane usiku,nilisahau kununua Christmas light duuu!! na maduka ndo washafunga. Ha!ha!ha!

 Basi sasa sisi hao kulala kumbuka masaa 4-5 kuna watu wataamka huko kumuwahi Santa Duuu!!! aisee nahisi ndo nilikuwa naanza kupata usingizi Mara Makelele hayo yanakuja chumbani kwangu Mum &dad,Mum & Dad  amkeni, njooni muone Santa ametuletea............(in English though ) yaani!!! unatamani upotezeae sema ndo hivyo inabidi uwajibike ha!ha!ha! 


 Yes walifurahi mnooo........ ila mwisho wa siku niliambiwa Mum i think santa forget to put the Light ha!ha!ha! Nikawambia nafikiri ameacha ili Mum & dad wanunue. So maduka yalipofunguliwa Baba yao alienda nao kununua hizo taa zakizushi zimeshukaje bei sasa????? na vijipambo kidogo . wakaja nyumbani na wao wakijisikiaje raha kuupamba mti Ha!ha!ha!

 JAMANI WATOTO WANAENJOY VITU VIDOGO MNOO ............. SA NYINGINE HATA HUWEZI KUVURUGA BAJETI YAKO............KIKUBWA NA WEWE JIWEKE WEKE KITOTO TOTO HIVYO HIVYO HASA KIPINDI KAMA HICHI 




ndo mjue story ya camping ilipoanzia......

 Wamesema Santa amewapendelaje sasa kila walichoweka kwenye list amewanunulia ha!ha!ha!


 hivi kwani miavuli humu ndani hamna hao ndo watoto bwana ????


Kweli Santa is the Best Ha!ha!ha!ha!

 Baba wawili katisha eti na mimi mpenda Nandoz zawadi zangu ndo hizo ha!ha!ha!ha!

Tunawapenda

Monday, December 29, 2014

LA FAMILIA....................

 Haya wapendwa wangu bila shaka sikuu zilienda poua eti eeeh!!! huku kwangu for the last two weeks ni full kusherekea , yaani maliko kibao mpaka mingine unaitafutia sababu ya kutokwenda..........  Kiukweli tunamshukuru Mungu mno tuko kwenye nchi za watu lakini duu!!! sometimes tunasahau kabisa kama tuko ugenini... Mungu anatumia watu aisee!!! Ila sema ndo hivyo ile harufu la pilau la uswahili huisikii ha!ha!ha! sometimes inabidi mimi ndo nijipikilishe nilipeleke ha!ha!ha! wanalipendaje sasa??? Anyway, kuanzia Boxing day mialiko yote kwishenea Ha!ha!ha!ha!  Tupo nyumbani michezo yooote imeisha.  kuna kajistory ntawapa nikitupia picha za boxing day ...... Tatizo Baba wawili kanivuruga hizi picha zilikuwa za episode 2 ye tayari kazivujisha facebook basi sasa nimeona tuanze mbele then turudi nyuma ha!ha!ha!ha!

 Sasa baada yamichezo watoto wanalilia camping kisa wamenunua hayo mabegi.... Tukaona isiwe shida ngoja tudrive somewhere ambapo watu huwa wanafanya camping tukaigize km masaa kadhaa waridhike turudi zetu



 hapo chacha ndo tushafika
 ufundi sasa unaanza

 waliangaikajesasa jinsi yakufunga hizo tent ha!ha!ha!

 Ngoja mama yanu niwasaidie

 duuu!!1 na mimi nachemka sasa


Bora tuteam up bwana  huku matukio yanachukuliwa bila kujielewa chezea Careen wewe.....



Hizi tabia za Mkeo anatoa maelezo we unampotezea ujue humtendei haki???? basi sasa endelea mwenyewe....

 Hatuja kaa  sawa hello mate (In Aus....) Do you need some help?? ee Bwana mi napenda  mzungu yule originaleee aisee ukikutana nae mbona kama uko home??? hana tofauti na yule mtazania wakijijini ukarimu jinsi mambo yao wanavyofanya aisee mbona utapenda!!!! achana na hawa wavamiaji kama sisi  aisee!!! nyodo kama yule mtanzania (kinasisi)  aliyetoka mashambani kaingia mjini  Darisalaaaama Duu!!! 

Mi nakwambia mpaka nilifikia niliona aibu wanangu wanavyofanya mambo yao ha!ha!ha! nimesema hawa nikija likizo tuu cha kwanza njombe au makete huko wiki nzima  yaani udaresala mwingiiiii!!!! ha!ha!ha!
l

eee bwana nikamkumbuka na marehemu Babu yangu mweee!!!! 


Wanangu sasa hili eneo ndo linanifanya kupeleka bush kwanza wanangu yaani hata kama huvijui unatakiwa kukataa kidizaini yaani mtoto kakunja sura yaani utafikiri kaona iny.....!!! halafu anatoa makavu kabisa!!! we ngoja udarisalama hapa kwangu marufuku wanahitaji mwaka mzima bush..... Ha!ha!ha!ha!

mchumba amekazana anawaonyesha manjonjo mara kwenye maji mara kuvua hao yabbies duuu!!!


Ule oroho wa maji kuomba nguo za kuogelea sikuusikia kabisa zaidi yakusikia Mumy how comes this water is very dirty(In Careen's Voice)
 Kidogo nimwambie Dad yako kajifunzia kwenye maji kama haya Ng'ombe anaogelea na yeye humo humo Ha!Ha!ha! uuuwiiiii!!! nyie msinisemeleee mwenzenu Ha!ha!ha!

Mama mtu wee naomba hiyo picha ipigwe haraka nimwachie huyo kiumbe  na huyo ndo wifi mtu hapo chacha!


 Tulienjoy kwa kweliiiiiiiiiiiiiiii......


 Mutu na Mubebe wake.............



Team.... Mume mtu yule kule nyuma yake........ Am sorry guys sio vizuri kumzungumzia but nimeona nimeguswa kutumia mfano hasa ukizingatia watu mko kwenye maproject Ha!ha1ha!
Ahsante Bwana Yesu yale makelele ya Camping sasa yamepungua ingawa wanasema wanasuburi yakulala huko huko  ......... Mum and dad make sure next time we go where there is no ants so we can sleep...... hi1hi!hi! mnamjua nani huyo eti eeeh!!!

Future Christina Shusho


Hapo chacha!!!



La Family

Tuesday, December 23, 2014

MAJANGAZA..........

Wandugu ni kweli  mtu kaitengeneza??? Duu aliyenitumia namwamini ila nawasiwasi asije na yeye akawa kapewa desa siyo mmmmmh!!!

Kama kweli na maswali meengi mno ndani ya nafsi yangu tatizo nikiyatoa tuu ntajikuta na hukumu. Ninachoweza sema ndugu zangu jina la Bwana halidhihakiwi...............

Kwa hili Pop corn zinahusika  na Bwana yuko kazini only kama ninachokisoma kimeandikwa na Muhusika.Acheni watutukane, Acheni watudhihaki, maana tumeamua wenyewe kuaibisha mwili wa Kristo.................

KAULI YA FLORÀ MBÀSHA KUFUATIA KUDAI TÀLAKA RASMI:
Nimefikia uamwuzi wa kudai talaka kutokana na kuchoshwa na vitendo vya ukatili nilivyokuwa nafanyiwa na mume wangu, kwa zaidi ya miaka8 na hata sasa bado anaendeleaje, Kwani hata kuongea uongo kwenye media juu yangu ni ukatili pia.. nimekuwa nikinyanyaswa kijinsia na mume wangu na sikuwahi kutoa taarifa mahala popote kutokana na vitisho alivyokuwa akinitisha. Watu Wengi wanafikiri nilikuwa na ndoa nzuri sana lakini kumbe nilikuwa Nikivumilia tu Kwani niliamini IPO siku atabadilika maana nilimpenda sana mume wangu.. Nilijaribu kuficha huzuni na maumivu yangu kila nilipotoka na mume wangu kwenda kwenye Huduma au mahala pengine penye mkusanyiko wa watu. Sijawahi hata Mara moja kutoa taarifa hata kwa wazazi wangu juu ukatili niliokuwa nafanyiwa na mume wangu.. Kwanza sikutaka kumvunjia heshima kwa ndugu zangu na pia alikuwa akinitishia kuniua na kuongeza kunifanyia ukatili huo.. Kutokana na historia yake ya nyuma alikuwa na uwezo wa kunifanya chochote na ndiyo maana nilikuwa nikimwogopa sana.. Siku zote nilikuwa akilala na panga kitandani ambalo ndilo alikuwa akinipiga nalo na kuapa kunichana chana Mwili Kabla ya kuniua.. Kipigo hicho nimekuwa nikikipata hata ninapokuwa kwenye Huduma bila kujali natakiwa kuwa kwenye mood nzuri ili ni perfome vizuri. Nimevumilia muda mrefu lakini ndo mateso yakawa yanazidi na kufikia hatua ya kufukuzwa akidai yeye ana mwanamke mwingine wa dini yake ya zamani Hivyo anataka amlete hapo nyumbani.. Nilikataa kuondoka na kumwambia amlete tu, tutaishi wote mimi nitakuwa nikilala chini maana nshazoea siku zote Amekuwa akinilaza chini . alivyoona siku zinazidi kwenda na mimi nimegoma kuondoka basi akaamwua sasa isiwe siri ya chumbani tena Akawa ananitoa ananipigia sebuleni na anasema nataka mtoto na wengine wote wajue kuwa huwa nakupiga humu ndani.. Ikafika hatua anataka kunitoa nje ya geti ili majirani wajue kuwa huwa napigwa na anifukuze mbele yao..
Kwa Miaka yote alinizuia kufungua account bank na kudai kuwa yeye ndo Mwanaume Hivyo pesa zote ataweka yeye. So pesa zangu zote nilizokuwa naingiza alikuwa akichukuwa yeye na kuzihifadhi kwa account yake binafsi.. Sikuwa nikibaki hata na mia.. Nilijaribu kufanya biashara lakini napo pesa zote Akawa akichukuwa yeye ikabidi niache.. Nikitaka hata vocha ya mia tano Lazima nimwombe hela na niitolee Maelezo ninampigia nani. Mume wangu kwa kipindi chote hakuwahi kuwa na kazi yoyote zaidi ya kunifanya mimi ndo biashara yake. Lengo lake ilikuwa ni kunitumia mimi kwa maslahi yake na sio upendo kama mke wake. Hakuwahi kunipenda hata yeye mwenyewe hukiri kuwa alinioa tu basi ili afanikiwe kwenda ulaya kwa kuwa mimi nilikuwa nikisafiri na babu yangu.. Na yeye kila akijaribu kwenda nje anashindwa. Kuna mambo mengi ya ukatili aliyokuwa akiyafanya ndani siwezi kuyasema kwa ajili ya maadili na pia bado Ninamheshimu kama mzazi mwenzangu. Alipoona siondoki pamoja na vipigo, matusi na kunifukuza kote.. Akasema nitahakikisha nakufanyia jambo ambalo utaondoka mwenyewe humu ndani bila kupenda.... Sitaki kuzungumzia swala ambalo liko mahakani ingawa hilo nahic ndilo alilokuwa kadhamiria ili tu niondoke. Nilijaribu sana kumsihi tukae kikao na wazee ili watushauri na kutusaidia lakini nilikuwa nikiambulia matusi tu ya nguoni ambayo siwezi kuyaandika hapa.. Siku niliyoondoka nyumbani alidhamiria kuniua alidai hata akiniuà hakuna atakaye amini kuwa ni yeye kaniua, na ni kweli maana sikuwahi kushtaki mahala popote. Alichukuwa panga akanipiga nalo kisha akaniniga Hadi nikaishiwa nguvu . Aliponiachia sielewi nilitokaje ndani. Ugomvi mkubwa ulitokana na mimi kukata kufanya tenda la ndoa kinyume na maumbile. Amekuwa Alinipiga na kunilazimisha kufanya tenda hilo kinyume na maumbike kwa Miaka msingi lakini nikisema bora nife kuliko kutendewa ukatili huo.Amekuwa akidai kuwa wanawake tumeumbwa ili tufanyiwe tenda hilo la ndoa mbele na nyuma so ni haki yake..
Niliondoka kwake nikiwa na sh elfu mbili tu. Nilimwachia kila kitu nyumba gari na pesa zote zikiwa kwa account yake zaidi ya milioni 50.
Sikuwa na uwezo wa kutoa pesa maana ni account yake binafsi.. Nimejitahidi sana kumwita kwenye vikao hata vya familia ili tu tujaribu kuzungum za lakini Amekuwa akionyesha dharau tu na kusema yeye haitaji ndoa tena anaoa mke mwingine Hivyo Hawezi kusuluhishwa. Ingawa Amekuwa akidanganya sana kwenye media. Nilimwuliza Unapata faida gani unapodanganya watu kuhusu mimi.. Akasema yeye amechafuka kwa ubakaji so acha na mimi nichafuke na akasema atahakikisha sifanyi Huduma sehemu yoyote labda nihame nchi. Kama msg hizo angekuwa amezituma bila kuandika na matusi ningezikopi but zaidi kauli zake ni za matusi. Hivyo imefika mahali nimeona bora tuachane kisheria na pia nipate haki yangu maana mume wangu anajivunia Mali ambazo hakuzitolea jacho yeye na huku anawatapeli watu kwa kudai kuwa hana pesa maana mimi nimeondoka nazo wakati ni uongo mtupu. Mimi ninapanda daladala siku hizi sababu sina uwezo wa kuwa na gari Hadi niazime kwa marafiki zangu. Mume wangu amekataa hata kumsomesha mtoto sasa hivi nahangaika kutafuta ada ili mtoto arudi shule lakini pesa yote anayo anayo mbasha. sasa sijui hapo ananikomesha mimi au mwanaye.!maana urithi wa mtoto ni elimu bora na mzazi anayempenda mwanaye atapambana ili kuhakikisha mtoto anapata elimu bora.
Nilikaa kimya muda mrefu sikutaka kuzungumza lakini imefika mahali Nimechoka maana huyu bwana hajiheshimu. Tukikutana anasema sio yeye anayepeleka habari mitandaoni..
Ninaomba wanaume wenyewe Mfano wake waache kuwafanyia ukatili wake zao majumbani .. Najua wako Wengi sana wanao nyanyasika kama ilivyo kuwa kwangu lakini Hawana sehemu za kukimbilia Hivyo wanavumilia tu na mwisho wa siku wanakufa na kuacha watoto wakiteseka. Mimi Nilivumilia zaidi ya Miaka 8 lakini imefika mahali enough is enough. Maandiko matakatifu yanasema, ndoa haivunjwi isipokuwa kwa uasherati. Acha nife kwa mapenzi ya mungu na sio kwa mapenzi ya mtu.. Na ni naamini sitakufa mpaka ndoto zangu zitimie.. Mume wangu ameapa kuwa atahakikisha sifanyi Huduma tena.. Lakini ninasema katika Jina la YESU, kama Bwana aishivyo, mwanzilishi wa Huduma yangu ni Mungu Hivyo mmalizaji wa Huduma yangu ni Mungu mwenyewe. Na sasa ninajipanga kumwimbia Mungu kama sitaimba tena.. Wakati mwingine usipokuwa mwangalifu ndoa inaweza kukukosesha ufalme wa mbinguni hasa Uki ingia kwenye ndoa isiyo sahihi. Ninampenda sana mume wangu lakini ninampenda Mungu wangu zaidi. Ahsante..
Nimeamwua kuandika Maana Nimechoka kuficha maovu aliyokuwa akinitendea.. Nimemtunzia heshima muda wote maana sikutaka jamii imjue ni mtu wa aina gani but yeye anatumia ukimya wangu kama udhaifu so naona bora niweze wazi ili jamii imtambue
Mimi yamenikuta najua Wapo Wengi tu wanapitia mateso niliyoyapitia mimi.. Kutokana na vitisho wanaendelea kunyanyaswa. That is not fair kwa kweli.. Mimi ningekufa Kabla ya wakati wangu lakini namshukuru mungu Niko hao hata sasa.
Na pia ili kuwaonya wanaume wanaume wenyewe tabia kama yake.. Kama umemshoka mwanamke achaneni kwa amani sio kumnyanyasa mwanamke kama alivyokuwa anafanya mbasha kwangu. Ninapinga vikali unyanyasaji wa wanawake na watoto majumbani.

Monday, December 22, 2014

PASTOR DARRYL BIRTHDAY PARTY........................

 EVENT: 70TH BIRTHDAY  PARTY 
                                  
ORGANIZER: NEITA,MISHELL,LISA & ROSE

MC: ASHLEY

DECO: NEITA,MISHELL & ROSE

COLOUR: BLUE&GREY

VENUE: STEVE & MISHELL HOUSE
Yes we love you Pastor........


yuuuuuuummmmmmmmm!!!


surprised face........




 Some people need to confess Ha!ha!ha!ha!  why would you do this to your Dad???

 Real!!!  how can you do this to you lovely husband???? Ha!ha!ha!ha! 


Steve & Mishell


The Burge's


Luke & melody

Pam


The maramba's



Neita
Lovely couple
The king himself and Gorgeous wife.........
Awesome people.

Speech Time

Terry
Thanks to everyone in  the church for your Generosity. and special Thanks to LISA FREETH DESIGNS 

Making sure!!! Thanks Lisa.

Holiday yeah!!!!

The End.........