Kwa wale wadau wangu mnaonifuatilia, kama mtakumbuka niliwahi kuzungumzia, jinsi gani nilivyoteseka miaka kadhaa iliyopita kwa habari ya wanadam fulani fulani, Ambao baadae niliweza kulielezea kwamba wakati niko kwenye mapito hayo nilidhani tatizo ni wanadamu hao kumbe tatizo ni mimi mwenyewe.
Nikasema ,Binadam tonatofautiana sana kitu ambacho mimi kipindi hicho sikuweza kuiruhusu akili yangu iamini hivyo., Labda kwa ajili ya makuzi niliyokulia, mazingira niliyoishi na vitu kama hivyo.........
Ngoja nikupe mfano, niliwahi kuamini unaposema huyu ni ndugu nilitegemea mengi, kuliko, isivyo kwa ndugu. Na kumbe!!!!kunauwezekano mkubwa asiye ndugu akakufaa kuliko ndugu. Neno ndugu kwangu lilimaanisha kabila,taifa,ukoo n.k yaani nilipokuwa na deal na taifa mbalimbali nilitegemea zaidi kwa Mtanzania mwenzangu kuliko kwa mtaifa mwingine, nilipodeal na Mtanzania,nilitegemea zaidi kutoka kwa ndugu wa damu kuliko kwa rafiki au jirani au mtanzania yeyote yule ..................... Nafikiri mnanielewa, na kwa kusema hivi naomba nieleweke sijasema NI KOSA endelea kunisoma chini utanielewa.
Nasikitika kusema kwamba kwa kipindi fulani matarajio yangu hayakuwa hivyo, Mbaya zaidi nilikuwa mwepesi sana wa kulia (maumivu yake usiombeeee).Nililazimisha sana kumbadilisha mwanadamu, nilitegemea mzigo ninao ubeba mimi juu ya ndugu yangu(rejea maana yangu ya ndugu) nilitegemea na yeye atabeba kwa uzito, na kama ni maumivu na yeye ataumia vile vile ..........
Wandugu hii ilinitesa sana nakumbuka kama nimaombi nilioooombaaaa ,mpaka, nilianza kuamini kuna maombi mengine Mungu hana uwezo nayo maana kila nilipoomba ili kudumisha yale mahusiano ndo kwanza nilikuwa naharibu, Nilitumia akili zangu sana mpaka nikaanza kuishi maisha yakuigiza ili tu niweke mambo sawa.Ndio kwanza niliharibu. Nilijikuta naishi maisha yakinyonge ndani ya moyo wangu, kwani maisha yangu binafsi yalikuwa hayana tatizo lakini ilipofika kwa jamii haikuwa kivile.
Siku isiyokuwa na jina akili ilinijia, sijui ilikuwaje (ni Neema) nikajikuta nawaza, tatizo sio jamii tatizo ni mimi. Nategemea zaidi kwa wanadamu kuliko kuwa na kiasi. Nikajikuta najisemea MAANA YA UNDUGU ninayoijua ni KWELI ila kuna namna inipasayo kudeal nayo...............Ilinibidi nifanye maamuzi, Haikuwa rahisi aisee ee!!!!! Nilijikuta nimeanza kuvaa vazi fulani ambalo kwanza sikutaka kunibadilisha uhalisia wangu. Ningeweza kukueleza mengi hapa ila baadhi mnanielewa hasa wadau wa siku nyingi.
Kuna kipindi sasa baada ya kukubali hilo vazi nilianza tena kujitathimini nilihisi kabisa huu sio mpango wa Mungu, maana nilijiona ile nafasi ya unyenyekevu,kupondeka imetoweka, yaani sinayo tena!!! zaidi nilijikuta mtu wa ujasiri mwingi, nilijiona niko proud sanaa LAKINI kila nilipojitathimini nilisikia sauti ikiniambia (unyenyekevu,kupondeka haimaanishi hali ya unyonge na kukupa maumivu bali, ni namna fulani ya hekima ambayo mwisho wa siku inakupa amani nakutokujutia.
KWA NINI LEO NIMEKUMBUKA HILI
Juzi kati kama kawaida yangu napitia madeni nikajikuta kuna $550 nilikasahau kama miezi miwili hivi, ila kwa sababu mteja mwenyewe ni the big boss, nikajua sio shida hata yeye amesahau ngoja nimkumbushe. Nikanyanyua simu nampigia duu!!!! jamaa naona kichwa hakikuwa sawa, aisee alipa ma f words yakutoshaaa!!!!! yaani nikabaki nashangaa kwenye simu nilichoambulia ni kimoja tuu kwa nini namdai wakati ameshanilipa??? nilimkatia simu, nikaanza kuwaza hivi amepata ujasiri upi kunifanyia hivi kwenye simu yakiofisi?? kwa nini anitukane hata kama pesa kaweka, kuna mengi yaliendela hapo huwezi amini. Nikajikuta kwanza nimekaa namwambia Mungu sitaki kukumbuka kilichotokea, ila haki yangu naipataje?
Kilichofuatia ndicho kilichonikumbusha hayo yote.
Nilijikuta nimelia tena!!! jinsi nilivyokuwa najiskia enzi zile ile hali ilinirudia tena wapendwa.............Jamani nililia kama mtoto.
Haikupita nusu saa nikajikuta natoka nje ya ofisi huku nikiwa nawaza yaliyonitokea, Mbele yangu nikamkuta mwanamke ninayemjua ameshika bunch of flowers anakuja. Namjua kama ni mfanyabiashara na pia huwa namuona kanisani, zaidi ya hapo sina ukaribu nae wowote. na kwa sababu hapo zipo kama ofisi tatu nikajua amepotea anaenda kwenye moja ya ofisi. Hivyo nimekaa mkao wakuulizwa swali kwa habari ya ofisi anayoitafuta. Sikuwahi kuwaza kama hata anajua ofisi yangu ipo hapo. japo moyo wangu unamawazo nilianza kuuandaa ili mawazo yangu yasimuhusu mgeni ( rejea nilipojifunza kujitegemea bila kutegemea akili ya mtu mwingine (TUWE NA KIASI CHA MATARAJIO)
Mara nikamsikia akiniambia huku akinipatia lile UA akisema, nilikuwa nafanya shopping mara nikasikia moyoni ninunue ua nije nikutie moyo, kuna sifa nyingi hapo alinimwagia akili yangu ikawa bado hailewi!!!!!! nilijikuta natoa chozi aisee, kati ya watu ambao hawaelewagi thamani ya maua mimi ni namba moja !!!!!!!kwanza huwa naona wananichanganya tuu, mtu akinilitea UA, Lakini Ua hili liliniletea maana kubwa, Binafsi mimi niliamini Mungu kamtuma maana alikuja kwa muda sahihi( Wapendwa mnanielewa hapa) lakini kilichonishangaza ni zile sifa ambazo kwanza sikuwahi kujua mtu kama yeye anaviona ndani yangu,Pili sikuwaza kama vinaonekana hivyo kwa wanadam zaidi ya familia yangu, Na vingine,hapo kale ndivyo nilivyokuwa nahitaji labda mwanadam aelewe lakini mapokeo yake yalinijeruhi, ki ukweli!!!!chozi langu lilijiuliza meeeengi!!! Ilibidi nifunguke maana naona hakunielewa kwa nini nalia vile. Aiseee kwa sababu ni mfanya biashara wa siku nyingi alinipa experience zake nikajikuta mbona langu cha mtoto???? Nilipata faraja mnooooo.!!!!
Nilichotaka tujikumbushe na tujifunze kuna kitu unaweza ukawa unakipitia ukadhani ndivyo kinavyotakiwa kiwe kumbe sivyo, mara nyingi jaribu kujiangalia mwenyewe ujue ni namna gani unaweza kujitoa (hekima itumike) bila kupoteza uhalisia. Mara nyingi Shetani huwa anatumia kile cha thamani ulichonacho kwa namna nyingine.
Guess what???
Baada ya hayo Tuligundua The boss aliweka pesa kwenye account ya mtu, na huyo mtu kajichunisha akidhani muujiza (kwi! kwi! Kwi!) The boss mwenyewe, alihakikisha pesa imeingizwa tena kwenye bank account yangu, Jamani hakusema samahani ila kule kushuka alivyoshuka na kujieleza kwenye simu. kwangu ilitosha nanilimshangaa sana Mungu kwa hilo .
Halafu unajua nini liliruhusiwa kwa sababu eti eeh??? na cha mwisho kikubwa wale ndugu,jamii,rafiki nimejikuta mahusiano yapo,tunapendana na kuheshimiana (niaminivyo mimi). kwani kwa sasa nahisi i expect only less or non!! na ninathamini na kuheshimu vyovyote itakavyo kuwa maana Wanadamu Tunatofautiana.
Duuu!! nimeridhika sasa maana hata leo nilitaka niwachunie ila hayo masumbuko ya moyoni nisinge lala.
Nawapenda