Pages

Ads 468x60px

Thursday, May 29, 2014

FLASH BACK..............................

Wiki mbili zilizopita mwenzenu nilipata ugeni,  ulioletwa na Christabell wangu (4yrs). Ana mwalimu wake wa daycare ambaye amekuwa akienda kwa miaka miwili sasa. Mwaka  jana alikuwa full time  ila mwaka huu anaenda once a week, kwa sababu sikunyingine anaenda shule........... sasa huyu mwalimu jamani alikuwa gumzo ndani ya nyumba aisee, mtoto ananiuliza maswali  meeengi. Mumy when are you inviting ...........???? ukiwa unamnunulia kitu akimkumbuka tuu, utasikia Mumy can we buy one for ..........., Mumy when she is coming for a sleep over???? hapo mezani tukikaa sometimes utasikia when ........ comes, she will sit here. Jamani kwa mda wa almost miaka miwili!!!! 

Ni kawaida yake aisee huyu mtoto akitaka kitu halafu usimpe majibu yakutosha  humnyamazishi, ni mwepesi kukuelewa kama  jibu lako limejitosheleza........... hata kama hujamruhusu kufanya atakwambia am not doing it coz my mumy doesnt like it, na atarudi kukwambia mumy .......... told me to do this n that but i said my mumy doesnt like it( kwa hapo Dada mtu huwa anakoma dogo anavyo mdispline). hii kitu nimeipata hata kwa walimu wake, mwalimu  asi introduce kitu kipya halafu yeye awe hawezi atamkalisha huyo mwalimu chini mpaka ahakikishe ameweza otherwise ni kilio.Akisha jua hanaga time na mtu.

 Sasa Mama yake nilikuwa nampotezea sana maswali yake ya huyu Mwalimu wake ila nilikuwa namtumia kwenye kumuandaa, ili asijicheleweshe namwambia leo unaenda kumuona mtu fulani weee!!! tutatumia mda mchache sana kujiandaa(kina mama mnanielewa eeh) mpaka hiyo siku ilipofika nimeenda kumpeleka  bwana,!!!!!!! nikamuona huyo mwalimu mie huyo kuogopa maswali nilivyoona anamkimbilia tu nikaomba kiss ya faster faster niondoke , sijafungua mlango wa nje nasikia Mumy,Mumy,Mumy wait ile kugeuka yuko na Mwalimu very serious ananiambia, Mumy now take ..............'s phone number, so you can ring to invite her to our house.(kuumbuana sasa maana sikupewa nafasi yakujitetea zaidi yakutimiza amri mda huo huo?)  na hiyo siku ikawadia  kama mnavyoona.

Hamna haja yakumuona huyo mgeni eti eeeh!! habari kamili ni juu ya mwanangu mie na ndio hiyo................. ntamkumbusha siku moja akikuwa jinsi alivyonishughulisha.
Mama wawili nilipumzika vile vishughuli vya mezani walihudumiana wenyewe kwa wenyewe
no pink plate & cup  kwa siku hii maana nilihisi ningeambiwa  na mgeni nimpe visahani vya kitoto maana nilivyosema leo mnatumia sahani hizi nilimsikia akisema yeah!! we are having the same plate like...........(mwalimu)

Hivi enzi zetu tulikuwa tunawashughulisha hivi wazazi??? hata sikumbuki aiseee lakini nilichojifunza ni hichi hizi nafasi zinasaidia sana kumjua mtoto.............

 ooh!!! sorry nimesema flash back nimejikuta naaandikaaaaaaaaaaaaa.

haya basi nawapenda



Wednesday, May 28, 2014

MAMA WAWILI..............

Kipink pink......................
 nani huyu????
kageuka......
spotted anajiweka tayari kwa picha.
 Mama wawili!!!!
Anawapenda mnooooooo!!!

Tuesday, May 27, 2014

THE LOOK............


Mama wawili
mapozi kabla yakuelekea
 nakomaa na weather soon vijigauni pia vitapumzika maana baridi inanipigaje miguuni???? mweeeee!!!


haya basi ilikuwa ladies Dinner.  once a month Mama wawili huwa natoka dinner na  wanawake wenzangu wa kanisani ( kiroho zaidi) huwa naipenda hii date aisee wanawake huwa wanafunguka aisee bila aibu.........kiukweli inatujenga mnooo kiimani na kimwili. 

 nawapenda

Monday, May 26, 2014

MAMA WAWILI

Pata muonekano wangu wa jana kanisani....................

blue..............
huyu hapa sasa
nimewambia vigauni hii week havikai kabisa vikilo vimepungua mweee .........check mikunjo hiyo!!! hiyo gauni nilivaa mwezi uliopita hiyo mikunjo haikuwepo kabisa!!!! duuu!!
weekend iliyopita nilikuwa kipink pink na kiblue blue.kila nilichokivaa kilikutana hizo rangi (except hiyo post ya kitaa iliyopita) sikupanga ila ninavyopitia picha nitoe post ipi nimejikuta ndivyo ilivyo. stay tune.......
nawapenda

Sunday, May 25, 2014

ABOUT KITAA....................

Nipogo watu wangu ni vile majukumu yamenizidi nashindwa kujigawa kuingia humu, kilichovuruga zaidi chaja ya camera nilikuwa siioni  na muda wakuitafuta ndo mpaka nitulie....... haya sasa ndo tushaiona matukio ya about to go, the look,........... mtaendelea kupata. halafu siku hizi sibebi Camera kwenye makusanyiko ni mpaka wahusika wahitaji  otherwise huwa naona hayawahusu sana si etiiii..........

my new magongo..........
herself
wandugu ubusy na stress za week hii vikilo vyangu kwishinea tunaanza upya kuvikusanya mweeee!!!!( kifupi Baba wawili nilikuwa naye mwezi mzima mzigoni so mambo mengi sana alinisaidia nikapumzika this week kaanza kufanya yake na yeye duuu ni full mchoko aisee, bado sijarudi kwenye mstari vizuri,not easy wandugu though i love what am doing......)

mazoezi ya miondoko nisije tia aibu kitaa.........
muke ya Slay

PENDA NYIE SANAAAAA!!!!

Wednesday, May 21, 2014

TUNAWEZA........

 Wandugu ule mpango wakuwezeshana, kama tulivyoamua kumuwezesha Mwanamke mwenzetu ambaye kupitia wewe  ndoto yake inaweza kufikia malengo fulani. Kama nilivyosema tangu mwanzo kwa habari ya huyu Dada yawezekana hana shida kama walivyo wengine  lakini ana ndoto. Ndoto yake inashindwa kukamilika kwa sababu ya hali halisi aliyonayo ( kama alivyotueleza mwenyewe) nikaonelea ni vyema kwa atakaye guswa kupanda mbegu ( narudia tena usitoe kwa sababu Mama wawili ametoa au amesema) hakikisha  kuna namna unayoifanya na Mungu wako akuruhusu upande mbegu na ikupe amani.kwa wanaoamini swala zima la utoaji mnanielewa hapa..............

huna naamini sana kumsaidia mtu mwenye ndoto ambaye najua siku moja atajisimamia mwenyewe, huwa nafarijika sana nikikutana na mtu  ambaye hayuko vizuri sana lakini anajikokota hasa kwa habari anataka kuwa nani ( kwa maana nyingine ana ndoto)..................... wandugu hata mimi ni muhitaji kuna watu ambao huwa wanatumika kwa ajili yangu, ninapozungumzia kumsaidia mtu ni yule ambaye mimi nimeandaliwa kutumika kwa ajili yake kwa kile kidogo nilichonacho.



 Ni hivi  mdau wetu alifanikiwa kupata kiasi cha shiling 500,000  kama mbegu kuelekea bajeti yake ya million 4.   na hapa chini ndo maelezo yake  hizo ........ nimeziweka mimi kwa makusudi fulani.

WITO WANGU KWA WALE MLIONIAHIDI KUUNGANA NA YEYOTE ALIYEGUSWA PLEASE INBOX NIKUPE NAMBA YA MUHUSIKA UFANYE KURUSHA......



Habari ya leo dada natumaini umzima pamoja na familia yako.
Nashukuru Mungu mbegu inaendelea vizuri na faida niliyopata nimeona ninunue printer hii inaprint inascan na pia inatoa copy ila copy kwa biashara hii haitafaa isipokua nitatumia kwa kuprint na kuscan. hivyo bajeti ya scan mashine ishapita. Mbegu iko pale pale bado iko kwenye mzunguko kama nilivyokuambia kwamba ................................ faida ninayopata nanunua kidogo kidogo naamini kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nitakuwa na ofisi kabla ya mwaka kuisha. Nashukuru sana na mwenyezi Mungu akubariki.

Salimia familia yako. 


USED PHOTOCOPY MACHINE
                   1,000,000
COMPUTER

PRINTER

LAMINATION MACHINE

BINDING MACHINE
                   1,000,000
CUTTING MACHINE

B. CARD CUTTING MACHINE

OTHERS

STATIONARIES &OTHERS
                      500,000
REN PER YEAR
                   1,200,000
UKARABATI AND SHELFS
                      300,000
TOTAL AMOUNT
                   4,000,000

Hiyo juu ndo bujeti


faida ndo hii.

Monday, May 19, 2014

MAMA WAWILI



Ukiona hivyo kipya..................
spotted!!!
Dada yenu..........(haya basi mdogo wenu)

muke yake
tafakari
haya nawapenda!!!

Friday, May 16, 2014

IT'S FRIDAY.........YEAH!!!!!!!!!


Sikia nikwambie,Jaribu lolote linalotokea kwenye  maisha yako, chunguza  kwa nini limetokea... ukijua  sababu ni wewe mwenyewe  hebu chukua hatua yakutubu, na kurekebisha... unajua nini mimi naamini sana ule msemo wa majibu hapa hapa dunia nikiingia kaburini huko ndo kuna hukumu ya wapi nastahili kwenda. so kuna vitu kwenye maisha yangu jamani huwa vinanitokea and i feel the pain mwisho wa siku nakumbushwa ,unakumbuka ulimsababishia someone pain kama hii???sasa ni wakati wako............unajua nini nimejifunza kukubali wakati kama huu maana ndio wakati pekee ambao huwa naamini  ni wakati wakujitathimini  kwamba mimi ni mtu wa aina gani, wapi maneno na matendo yangu huwa hayana kibari japo huwa najiona niko sawa,huu ni wakati ambao kiwango changu chakupondeka kinakuwa maana nimetambua na niko tayari kurekebishwa,na pia ni mda ambao huwa unanipandisha kiwango cha kiroho maana huwa najitahidi sana kuutafuta uso wa Bwana ili nijue natokaje sasa maana kuharibu ndo nisha haribu(KUBAKI NJIA KUU NO MCHEPUKO).................mwisho wa siku najua MUNGU ni mzazi wangu anayeniadhibu na kunirudia( wasomaji wa neno mnanielewa hapa)

 lakini,

unapojichunguza ukaona kabisa hilo jaribu limekuja kwa mlango ambao hauonekani ( bila kulazimisha haki).Akili yako imefika mwisho huelewi  Mungu akupe hekima hapa jinsi yakusogea mbele zake kwa habari ya hilo maana,( Angalia usije kuwa kama mfarisayo aliyejigamba.........Luka 18 soma yote tuu kuna mengi yakujifunza hapo)  Vinginevyo mpendwa chill out....... Bwana yuko kazini...... kupaniki kwako,huzuni zako, lawama zako,manung'uniko yako,stress zako HAZIBADILISHI MPANGO WA MUNGU .......  ni kweli imeandikwa Bwana atafuta chozi lako (jiulize chozi la manung'uniko, chozi lisilo na imani hata kidogo?.........) Bwana anataka uelewe ameruhusu kwa sababu, na yeye ndie akupae neema yakulishinda kwa  maana, Bwana ameandaa MKATE MBELE yako.

 NIKIKWAMBIA UJUE NIMEPITIA NA NINASHUHUDA JUU YA HILI yaani ni  NO LONGO LONGO wapendwa. kama hapa nina liushuda hilooooooooo ila kulisema nasubiri Mungu aniruhusu nikushirikishe.

Otherwise mimi nawapenda mnoooo aiseee dont forget IT FRIDAY YEAH!!!!!!!!!!!................
Jamani fashion ya kucha nimeona inipite mpaka vacation or long weekend, nature ya kazi yangu imegoma kabisa...... nimejikuta siku za jumatatu  nateseka sana kubandua na mara nyingine najifanya Boss lady ofisini uzalendo unanishinda (najikuta na act kwa sababu ya kucha lol) nikitoka nje nikaona mzigo unaotakiwa upigwe duu!!!! gafla uzalendo unanishinda hahahaaaaa!! yaani hapo hata nikikosa kiwembe ntang'ata kucha mpaka nishike jembe.................(mtoto wa mkulima ni mkulima tuu hata  aingie mjini atalima bustani).
be you
sijui napenda rangi gani za nguo ila nikiwa nimetupia black huwa najipenda zaidi.
mapozi mengine hata sijui nayatoga wapi????

mubarikiweeeeeeeeeee mpaka mchanganyikiweeeeeeeee

Wednesday, May 14, 2014

THE LOOK

Ignore hiyo garden yetu huko nyuma ha! ha! ha! Tuliweka swimming pool ya watoto tulivyotoa  garden ilikuwa ina rangi nyingi , so tumeachia iwe msitu kiaina ili tukikata iwe rangi moja............. kama umefuga mbuzi au sungura karibuni kwangu mlo upo wakutosha kama mnavyoona ha! ha!ha!(joke)
msisahau sinaga outing monday to thursday za kunivalisha hivi.........busy kuosha magari ni full kisela sometimes naonekanaga kama teja ( full mlegezeo,kofia na buti hata muondoko sasa wa kijeshi maana muda wote nina haraka............. ) labda itokee nina ishu za kiofisi..........muonekano huu wa last weekend

myself


mbarikiwe........

Tuesday, May 13, 2014

MIMI HAPA..............

Tupogo wandugu msitake kujua kinachooendelea nyuma ya pazia duu!!! 



Black& white mix na rangi yoyote yakung'aa  huwa inakubali eti????

 na bado kabaridi kakuongea na moshi mdomo hapo tuu kuna jua la umbari ......nione  hiyo sura sasa inavyosikilizia   baridi






Sunday, May 11, 2014

HERI YA SIKU YAKINA MAMA..............


Mi mwenzenu ndo nishaimaliza..........  Kiukweli  being a mother is a greatest privilege of all!!!!!  hata sijui nisemaje??? mbarikiwe all mothers out there. Tukumbushane tuu Wamama wote hili ni Jukumu aiseee, Leo tunaitwa kina Mama kwa sababu kuna waMama waliokubari kutumika kutuandaa hivi tulivyo, Mungu atusaidie na sisi kuwaanda wa Mama wajao  haijalishi una watoto wa jinsia gani ( kuna huu msemo unasema mtoto wa mwenzio ni wako) .........Jamani huwa sielewi kabisa  Mama anayemfanya katuni ,nakumchambua mtoto wa mwenzie tena malaika hata asiyeelewa chochote aiseeeee!!!!Hasira za wazazi unazipeleka kwa mtoto weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!! Narudia tena Mama ni jukumu na hilo ndio lililokufanya leo uwe special.Tuangalie sana kile tunachotamka kwa mtoto wa mwanamke mwenzetu hasa hawa wasioelewa  kitu  wandugu. oooh!!! Sorry wandugu nimehama gafla ha! ha! ha! haaaa.Hisia zimenijia unajua tena UMAMA.........

 Wapendwa wangu  woote mnaowish siku moja kuwa waMama, Mungu akaikumbuke haja ya moyo wenu Amini ipo siku na wewe utaitwa Mama. Sawa, Doctor amekwambia haiwezekani hizo ni sauti tuu za wanadam zinazokuthibitishia Wanadamu wanakikomo,usitegemee akili za mwanadamu yupo Mungu aliyesema hakuna Tasa,Neno lake huwa halijipingi yaani ni kweli na amina.Achana na historia tuingie kwenye uhalisia. naelewa ni neema kuhamisha akili na kuamini haya ninayokwambia maana hata  Sarah alisema Alicheka na kusema LITAWEZEKANAJE JAMBO HILI????  nimeshudia watu waliambiwa Haiwezekani na ikawezekana.  Wanadamu hii ndo asili yetu maana nakumbuka hata baba wa Yusufu alipopelekewa lile gwanda la mwanae alichoamini ni kile alichoambiwa, sidhani kama hata alikumbuka kwenda zaidi ya pale, hata kutaka kujua eneo la tukio ili japo akaone hata mfupa, basi hata nywele iliyodondoka ili kuthibitisha kile alichoambiwa na kuona.alichoishia ni kuomboleza na sidhani kama aliamini Bwana ameruhusu kwa ajili ya utukufu wake.................Hebu tuombe neema itakayotuwezesha ku AMINI,AMINI,AMINI INAWEZEKANA . ondoa hicho kipingamizi kinachozuia kutokuamini kwako ili uruhusu ile Nguvu na mamlaka itende kazi. Wandugu haya mambo yakiroho yanategemea sana nakuamini kwako.

HAYA BASI NAWAPENDA MNOOOO.
 lunch @Nandoz.............kijiwe chetu mara nyingi siku za jumapili mchana
About to go......

Mama wawili.
Jamani My Christabell ujanja woote huwa hawezi kunyosha kidole gumba kama baba yake hapo ukimstukizia atahangaika dakika kadhaa. ndicho kilichomfanya Mama wawili acheke mpaka Pengo lionekane.
ukimzingua sana anakasirika ha! ha! ha!  Dad anasema mwache afanye mwenyewe Mama huruma tena ha! ha1 ha! ha! uMama tena.........
 Mtoto mkubwa amewakilisha kikweli ukweli aiseee.Alijitahidi mnoo kuwapanga wanawe na kufanya vitu vilivyonifanya kweli nijivunie kuwa Mama.AM VERY VERY VERY PROUD OF HIM.  Yaani hii week nzima wanake wanavyorudi na vizawadi vya Mother's day (sijui wenzangu na nyie yamewakuta???mimi mwenzenu nimeletewa michoro miingi kuanzia jumatatu hata mingine siielewe zaidi ya pale walivyoandika Happy Mothers Day  na kiss kiss tuu meeengiiiii.......Walimu nao walikuwa na shughuli kweli kweli duuu!!!!) sasa  Baba yao anavyojitahidi kuwaelimisha waelewe nini maaana ya siku. Asubuhi mwenzangu kawahi kuamka na wanake  mi naamka watu wameshajiandaa na kunisuprise tuuu. NIMRUDISHIE NINI HUYU MUNGU KWA WEMA NA FADHILI ZAKE?????

Mutu na Mama ya watoto yake..........
The End.........