Nilichogundua ni kwamba wanadamu tumeumbiwa nafasi mbili. moja nikujitendea/kujihudumia mwenyewe na ya pili ni kujitendea/kuhudumia mtu mwingine.............cha ajabu ni kwamba wengi wetu tumejikita sana kwenye nafasi ya kwanza ambayo imetupelekea kuwa wabinafsi,na zaidi imetupelekea kutokujua nafasi ya wakati muafaka na jinsi yakukabiliana nayo, na tena imetufanya tuwe wanyonge,watu wakunung'unika,laumiana sisi kwa sisi na vitu km hivyo.tumetekwa na hii nafasi kiasi kwamba 24/7 tunataka kuwa sisi na kujihurumia kuliko pita kiasi............
Tumesahau kwamba kuna nafasi ya pili ambayo inatupasa kuipitia ili fulani apone,ili fulani ainuliwe,ili kusudi ukiokee kinyonge na kukipa furaha,ili kusudi kupitia wewe jamii ipate tumaini na ndio maana tumekuwa tukiwakumbuka wengi nakuwaita mashujaa.... tukimaanisha walipata neema yakujitoa kwa namna fulani kwa ajili ya wengine kwa maana nyingine hawa watu waliitambua hii nafasi ya pili nakujua nafasi yao nakuitumia kwa ujasiri........ nikisoma maaandiko matakatifu na muangalia Musa , nanukuu kutoka3:11("MIMI NI NANI HATA NIENDE KWA FARAO NIKAWATOE WANA WAISRAELI WATOKE MISRI?)
kwa jicho la Mama wawili, nahisi Musa hakutambua nafasi yake,yawezekana aliangalia ukubwa wa jambo lilivyo,au yawezekana alijihurumia hasa akimwangalia Farao na mamlaka yake,au hakujiamini kabisa ("TAZAMA HAWATANIAMINI WALA HAWATANISIKIA SAUTI YANGU") mpaka pale alipokubali na kuonyeshwa baadhi ya uweza uliopo ndani yake.
Hivi ndivyo tulivyo wanadamu waleo tumekuwa ni watu wakujihurumia kupita kiasi, tumeshindwa kutatua matatizo ( face challenges) kwa sababu ya ubinafsi cha ajabu tunajikuta kila siku tunaangukia kwenye hilo tatizo na halipati utatuzi kuna msemo unasema TATIZO HALIKIMBIWA ILA LINATAFUTIWA SULUHISHO. kama mimi mama wawili kuna kipindi niliangaika mno juu ya hili nilidhani njia pekee ni kuwa mbali na jamii au vitu hivyo vilivyonisababishia tatizo,na kukimbia kabisa cha ajabu Mungu alinipa mapumziko ya mda tuu na kunirudisha kwa kasi na kujikuta nimerudi nakufungiwa na mageti ikimaanisha hakuna kutoka mpaka KIELEWEKE ha! ha! ha! ila kikubwa baada yakujitambua amenipa amani ya hali ya juu kiasi kwamba ninaweza kuwajibika bila wogo, kujistukia, ujasiri wa ajabu yale maumivu niliyokuwa nayaona yamegeuka kuwa kicheko na mda mwingine yamenigeuza kuona huruma kwa muhusika hasa anapoona anafanya kwakunidhuru au kunikomesha au kwa namna yoyote inayofanania.........NYIE ACHENI MUNGU AITWE MUNGU BWANA............wasomaji wa Biblia mtanielewa na hasa tukimwangalia Yona alivyogoma bora afe kuliko kuendelea na wito aliyoitiwa.
Namwangalia Daudi pia alivyotambua muda na nafsi aliyonayo hasa pale mtoto wake alipomgeukia kutafuta roho yake akiwa katika harakati zakumkimbia mwanawe alitokea mtu wa kabila la Sauli aliyeitwa Shimei, kasome samweli wa pili 16:5......... nilichojifunza Daudi aliujua wakati alionao , angeweza kumfanyia chochote ila aliruhusu kulaaniwa, kutukanwa, na kuaibishwa.
Kikubwa hapa ninachotaka kusema matatizo yapo ( challenges) na yapo kwa sababu fulani kikubwa ni kutambua nakujua nafasi yako juu ya hili.
Namalizia kwa kumwangalia YESU mwenyewe aliposoma chuo cha nabii Isaya LUKA 4:18 .tukumbuke alikuja kama mwanadamu alipata maumivu km mimi na wewe alijua vita atakayoikabili,upinzani juu ya hayo aliyoyasema lakini kikubwa alijitambua na mamlaka iliyopo ndani yake.
HILI NI JICHO LA MAMA WAWILI