Jamani eeh mwenzenu nimechoka kujitetea yaani..... siku zinavyozidi najikuta na maliza project hii naingia nyingine. Ambazo zote nahisi zinahitaji Muda wangu halafu unajua nini??? Mama wawili karibu kila kitu kinamuangalia yeye inaweza kuwa full au half.....
Nina ndoto zangu km mwanamke, nina wajibu wangu km mwanamke,Mama na rafiki....Katika vyote hivi namshukuru Mungu amenipa moyo wa Marry sio wa Martha, wasomaji biblia mnanielewa hapa au labda niseme unapofanya kitu fanya km unafanya kwa Bwana..... ha!ha!ha! watasema najifagilia haya basi, wenyewe wanasema fanya kitu yenye roho inapenda..................
Mara nyingine huwa najioni ni mtu tofauti kidogo, nimejikuta na penda vile ambavyo labda wanawake wenzangu wengi hawavipendi nawaza tuu jamani sina uhakika lakini mwee ha!ha!ha!
Leo kuna kitu fulani kimetokea na uzuri nimepata kamda kakuja kuongea humu nimeona labda tutiane moyo.ngoja nijifagilie kidogo lakini ha!ha!ha!
Wanawake wenzangu ni hivi Mama wawili huyu anauwezo wakukaa nyumbani na kulea watoto na maisha yakaenda yaani...... Jamani eeh Baba wawili anafanya kazi mgodini....... halafu mjuege aliitwa kuja kufanya kazi na alikotoka alikuwa si pabaya.........
Leo nimisifa tuu humu ndani ili mnielewe........... Nikimaanisha japo kuwa nimekuwa nikitumia lugha ya mabox ni namna tuu yakutaka kuelewana na wale walengwa ninaotaka kusema nao, lakini kiukweli kweli uwezo wa kuishi nakulipa bills na haya mapicha yote mkayaona labda ninachoweza kusema sina uhakika kwenye nafasi ya maamuzi km ingekuwa hivi na haya maficho ficho ya mara kwa mara labda yangekuwa under bajeti sana.................. ninavyosema maamuzi sio yakununua soseji, nepi za watoto sijui uji wa mtoto nazungumzia maamuzi makubwa ambayo yaani ni makubaliano tuu kulingana na unachokiona.(kuna mtu atanielewa)
Na pia pamoja na hayo masifa yote hapo, km we mgeni humu ndani kwa miaka 6-7 niliyoishi huku ka cv kangu kana uzoefu wa kulea wazee,na kusafisha vyoo mpaka kufika
HAPA ........ labda nitumie hayo maneno ambayo kwa wengine huwa mnaona hayasemeki mbele za watu, achilia mbali kale kadegree kangu niliko kuja nako, japo kaliwahi nifanya niingie kwa ofisi ifananayo kwa mda wa less than week ha!ha!ha! chezea wazungu weye ..........no!no!no! ulikuwa ni mpango kamili wa Mungu aisee ...japo sikuuelewa ndani ya ile week ha!ha!ha! nilijionaje sifai sasa duu!!!
Sijamaliza misifa nasema hivi kabla sijaja mwenzenu nilikuwa ka afisa masoko kwenye ofisi fulani ya serikali na kumiliki ka mkoko kangu mwenyewe bila kusahau boutique Sinza kwa lemi, oh no! nimesahau nilipanga nyumba nzima sinza ha!ha!ha! rafiki yangu mmoja alikuwa ananiambia Bwana we si useme unakaa kwa mtogole??? Sinza gani vituo viwili mbele kwa mtogole ha!ha!ha! Lakini unajua nini maisha yale yakuwa tosha kuitwa toto la mji ha!ha!ha! cha ajabu maisha yangu mengi yalikuwa kanisani duuu!!! nahisi bado Mungu na akiba ya yale maombi duuu!!! hamna kitu najidanganya yale maombi yalikuwa yakusafisha uchafu wooote wa kabla ya neema ya wokovu maana duu!!!Mpaka leo huwa najitia tuu moyo na andiko linalosema sitaukumbuka uovu wako wooooteee..............Haya hivi unafikiri kazi kuleta heshima mjini?? ila sema nini nilitakiwa kufanya kazi ya ziada mitandaoni kujiweka karibu na mablogger,na wale wote watakaonifanya nionekane bila kusahau mapicha kuachia kila siku ha!ha!ha
Nimesema ni masifa day right???Mmezoea kunisikia nasema ni kwa Neema ha!ha!ha! Yes ni kwa neema lakini neema haiji km hujafungua mlango ndugu zangu.Nilikuwa namsikiliza T.D J jana anasema ("Do you want it bad enough to do what it takes to get it done???" )
Hichi kilio cha wanawake cha mitandaoni mi kuna wakati natamani kusema ila nashindwa ndo maana mkiniweka huko kwenye magroup najuaga lengo kubwa wanaoniweka labda wanataka nifunguke au niwe msaada eneo fulani, maana wengi wenu huwa mnakuwa wadau wangu humu ninaowajua lakini ,huwa inaniwia vigumu kwa maana sijui kusudi la yule muhusika kuanzisha hilo group ni nini?? limebeba watu gani?? na je ni kweli ntakachokisema kitamsaidia mtu au ndo kuharibu mpunga wa mwenye shamba??? so mtanikuta napita tuu kimya kimya japo kuwa huwa nawashwa haswa...................
Nimekutana na mada eti watu wanabishana jukumu la nyumba ni la nani? wengine wameweza kwenda mbali nakujisifia eti Mume wangu anafanya kazi ambayo inaweza kumfanya aishi nakulea watoto wake, kwa hiyo yeye haoni sababu afanye kazi ya nini..... Kha hii akili matope??? aisee mi nilianza kuhisi ametufanya wote mamburura wenzake, nilikasirikaje??? huko nikaogopa kutia neno kwa sababu hizo niliziweka hapo juu.Kilichonimaliza ni vile comments zilizoendelea zikawa km za kusapoti fulani, nakujazana ujinga (Mawazo yangu) na pale ndipo nilipojiona labda niko tofauti km nilivyosema hapo juu sehemu km hizi ukiona nimesema kitu ujue nimeharibu maana huwa siwezi kumridhisha mtu...............
Mi labda nifunguke kidogo namuelewa yule mwanamke mwenye watoto garama za kulipa mara nyingi huwa zinakuwa kubwa kuliko za kile utakachokipata.... au km ni tofauti basi ni ndogo mwisho wa siku wanafamilia inabidi kile kitakacholetwa ndo hicho hicho kitumike kwa bajeti.
Nilitamani kuuliza swali lakini kwa maelezo yake niligundua huyo mwanaume mwenyewe ameajiliwa yaani.... nilitamani kuuliza miaka mingapi amefanya hiyo kazi yakuajiliwa na ni kazi gani??? ha!ha!ha!ha! umbea tuu wakati kusutwa naogopa........ Nyie sikilizeni kwa nchi zetu hizi za ulaya ukiona mtu mpaka kwenye miaka ya hamsini bado yuko chini ya bosi na kwa sifa hizo za mitandaoni kujinadi eti anamaisha mazuri mmmh!!!mkimbie huna utakachojifunza hapo zaidi ya mashauzi ya mapicha ya kutry kuweka jina mitandaoni ha!ha!ha!ha!......am telling you (In Diamond platnum sauti ha!ha!ha!) kimbia aisee Beba jembe nenda shamba asikupotezee muda.
Tunataka kujua leo kesho huyo anayekulea akiondoka utasimamaje, basi haya unamsaidiaje huyu anayekulea km unampenda kweli kwa nini usimsaidie mwenzio in his 40's hayuko chini ya boss..... we bwana wee kwenye 50' watu wanataka kula bata sio kukurupushana mamaboss na basi uwe boss mwenyewe kwa sifa hizo............ nani hapendi???? eeeh nyie bwana mi ntaongea sana ila akili mukichwa na hii mitandao.............
haya nawapenda
mbeba mabox in a serious mood......
Mpiga picha tulia watu tujipange
Kwa heri wenzangu tulio nchi za watu mnisamehe nimeona tuwasaidie kidogo wenzetu tunawadanganya sana hadi huruma....