Sijui nianzaje hii, na wala sijui ntamalizaje......... ila ngoja tuu nianze kwa kutiririka vyovyote ilivyopangwa kuwa bila shaka itafika kwa mlengwa.........
Ni mwezi sasa au zaidi,hichi kitu kinanijia tuu..... yawezekana hapo nyuma kilikuwa kinakuja sina uhakika . Maana sikumbuki nilikuwa nakichukuliaje, ila kwa huu mwezi najikuta naweza hata nikajipa kamda kutafakari na kuwaza na wakati mwingine nahisi kama najibiwa.Sina uhakika maana mi nami kwa misifa sichelewi kusema Bwana kasema na mimi ha!ha!ha!ha! chezea upendwa wewe............ mwisho wa siku mi ngoja nifunguke mlengwa atajijua km nimemuuzia chai au nimechangamsha genge...........
Km mwezi hivi niliwahi kuona post moja huko mitandaoni, watu wanaishare sasa hapa nahisi naakili zangu zilijiongeza.
ujumbe unafanana hivi.
NUKUU
"KAMA MUNGU ANGENIBARIKI KIFEDHA MAISHA YANGU YANGEKUWA UTOAJI KULIKO KUJIONGEZEA GHARAMA ZA MAISHA"(kumbuka ni mtu anasema)
Haikuwa mara yangu ya kwanza kusikia......... wapendwa kujisemea nafasi ya mtu fulani kujilinganisha na mtu mwingine nakujiweka kama angelikuwa yeye angelifanyaje kwa kumaanisha yule muhusika ameshindwa kutendea haki ile nafasi yake.........
Mama wawili nalielewa sana swala la utoaji na kuliheshimu. Naelewa lina taratibu zake na mara nyingine sio rahisi kuonekana kwa macho yakibinadamu....... ikitokea limeonekana kwa macho ya damu na nyama huwa linakuja kwa namna fulani hivi ambayo muhusika anaweza asijielewe km liko hivyo. (nakosa lugha nzuri yakuelewesha hapa ila twende pamoja labda huko chini utanielewa)
Naomba nieleweke hapa sizungumzii vitu kama kuweka nadhiri mbele za Bwana au zawadi. kwa mfano unaposogea mbele za Bwana nakuweka nadhiri......... Bwana ukinitendea hili nitafanya hivi kasome 1samweli 11 utanielewa
au
tunaposema jamani tutoene ahadi kwa ajili ya ujenzi wa kanisa au jamani mshindi wa blog tutampa ......ha!ha!ha! nimecheka na kucheka hapa mnajua deni sijamaliza?? anyway tuendelee..........
Turudi sasa kwenye hiyo siku sasa(nukuu kule juu)
nilijikuta nawaza, Hivi kwa nini Mungu hakumbariki mtu wa dizaini hii, mwenye njaa yakusaidia ki hivi??? Je ni kweli Mungu anawabariki watu wasiotoa ili wajinufaishe wenyewe??? sina uhakika km nilipata majibu ndani ya siku zile zaidi yakujisahaulisha.....
Nina tabia moja nikiwa sielewi kitu nanikiona kitanipotezea muda wa kutafakari huwa najisahaulisha tuu kwakutafuta namna....... ila bahati mbaya vingine huwa vinagoma vinabadilisha style tuu yakuja ha!ha!ha!
Basi tena siku nyingine km wiki baada nikaja kutembelewa na mtumishi mmoja ofisini ambaye labda back ground zetu zakiimani zinafanana ha!ha!ha! nimeanza urangi hapa eti eeh!!!Biblia nimoja iwe mweusi au mweupe maandiko ni yale yale..........labda sijui niseme mapokea!!! hebu nielewe hili swali nililomuuliza labda utanielewa na maanisha nini........
Baada ya maongezi ya mda mrefu yanayoshabiana na maswali na majibu. moja ya swali nilimuuliza hivi inakuwaje unapofanya kitu kwa ajili ya Mungu(mfano fungu lakumi,sadaka ya shukrani,.......,.......) huku tuliko mtumishi anaweza kukushukuru je hii haiwezi kupelekea mtu akajikuta analewa sifa na badaye kujikuta anafanya kwa ajili yakuonekana???(kama hajakomaa kiroho) ha!ha!ha!
Alinijibu alivyoweza kunijibu na nilimuelewa......Tuliendelea mbele kidogo kukazia maongezi nikamuuliza sasa kwa mazingira km haya tutamsaidiaje huyu mtu, ambaye yeye haoni km wanavyoona watumishi waliokuja kumshukuru kwa habari ya jambo hilo alilotenda au analotenda, maana anaamini anafanya kwa Bwana kupitia watumishi wake asingetemea heshima juu ya hilo????(rejea niposema nakosa Lugha...........)
Kwa jinsi alivyonijibu tafsiri yake niliyoipata ndani ni hii
UKIMUHESHIMU BWANA NAYE ATAKUHESHIMISHA ila sasa, unatakiwa kuwa makini sana heshima nyingine unaweza kufungua mlango wakukutoa kwenye kusudi.........(nimesema hii nitafsiri yangu niliyoipata baada ya alichonijibu)
Hatukuishia hapo bado nafikiri kulikuwa kuna kitu ambacho kilitakiwa kipatiwe ufafanuzi, bila hata sisi wenyewe kujielewa....... Gafla alianza kunipa ushuhuda kwa habari ya watu mbalimbali jinsi walivyobarikiwa kalama ya utoaji... nikapata swali tena nikamuuliza ha!ha!ha! Je utajuaje km wewe ni mtoaji???? na kwa nini wapendwa wengi tumekuwa waombaji zaidi ya watoaji? aisee alinifungua vitu vingi mnoo..... niliamini hata yeye hajui km ananisaidia maswali mengi niliyokuwa najiuliza wiki kadhaa zilizopita.......
Kiukweli nilijiridhisha akili yangu kama kawaida yangu nikapotezea haha!ha!
Bwana nyie mi natumia mda mwingi bafuni nahisi nalipa bili kubwa sana ya maji kwa sababu yangu nikifungulia shower kunitoa unaweza hata kunisahau,napenda my long shower just before bed ha!ha!ha!(hamchelewi kitchen party eti nambania mtu mshindwe kazi km kawa kuna kuoga ile yakungojewa baada ya hapo chacha nikirudi bafuni ndo kwa nafasi kikikiii!) halafu sinaga cha maana ninachokifanya wandugu,yale maji kunimwagikia basi ntaawaza, ntatafakari wee mara nyingine km huwa naongea na mtu hata huwa sijielewi.........
Basi jana Bafuni yale mawazo yote yalinijia kuanzia siku ya kwanza mpaka siku yakuongea na mtumishi aisee!!!
mpaka namaliza kuoga nakutoka kuamua lazima nije nizungumze hili nilipata majibu haya
Wapendwa wengi sana tunapenda kujihesabia haki, Mungu anajua kwa nini ametuacha km tulivyo kwa sababu anajua akitupa zaidi hatutaweza........ labda tutapoteza kusudi kabisa...... hebu tujichunguze sisi wenyewe ni kipindi gani ulichokuwa mnyenyekevu mbele za Mungu?? kama sio pale ulipokuwa kwenye mabonde unahitaji neema ya Bwana ituvushe....... je unapojifananisha na yule mtu, je kwa hiyo nafasi ndogo aliyokupa Bwana umefanya nini? Ukigundua unajiona unafanya zaidi na ulichonacho nakujikuta ndani ya nafsi unajilalamikia nakuona unafanya zaidi na haikupi amani mi naona upotezee tuu yaani kwa maana nyingine unatafuta sifa za kimwili sio kiroho ha!ha!ha!kasome sadaka iliyokubarika mbele za Bwana ni sadaka ya namna gani..............(sijui lakini nimawazo yangu)
Tukamsome Ayubu. Aisee yule kiboko mpaka shetani aliomba kibari yaani....... maana aliamini labda anampenda Mungu kwa sababu yakubarikiwa kwake kumbe hata alivyokuwa chini kabisa alinyenyekea.........(natumaini naongea na watu wanaoelewa eti eeh) Shetani mwenyewe aliandika maumivu mwisho wa siku.Hebu tujiweke hapo tutaweza??
Nikiwa kule bafuni pia nilijikuta nimemkumbuka yule mwanamke malaya aliyewaficha watumishi wa Mungu( nimekosa mda kuchungulia nisome tena bila shaka mnanielewa) nilijikuta najiuliza hivi katika nchi ile ni kweli kulikuwa hakuna namna wale watumishi wakasaidiwa kivingine?? na sio mwanamke malaya??? maana nilihisi Yule mwanamke alijijua kabisa wao na yeye hamna kitu lakini ile roho yakujitoa bila kujali anamsaidia nani na mtu wa dizaini gani??!!! kuna kitu nilijikuta najifunza kupitia mawazo yangu
haya nakupa home work ukawaze na weweha!ha!ha! unajifunza nini hapa kupitia huyu mwanamke na kile alichokifanya kwa watumishi......
Kaushauri kadogo wapendwa nafikiri i vizuri kuomba neema ya Mungu kutuchunguza kwa habari ya eneo husika badala ya kujihesabia haki na kuweka lile neno Mungu anampa ampendae ha!ha!ha! Nalipenda sana neno la Mungu ila chacha wapendwa tunapotafutaga namna la kulipenyeza kwenye eneo fulani tunalopitia mwee!! kuna wakati huwa najicheka mwenyewe ha!ha!ha!
Wapendwa Mungu aliupenda ulimwengu ambao mimi na wewe tupo hivyo basi katupenda sote......... Kiwango na namna ya baraka inategemea na muhusika mwenyewe...... vinginevyo Bwana ka,sema hivi njoo tusemezane, leta haja zako..... kikubwa niuvumilivu na pia tujue ni kweli kuna miujiza lakini vitu vingine ni process lazima akupitisha eneo fulani kabla hajakupa eneo nyingine ipo hivyo yaani...........
Khaa hata sijui km nimeeleweka ha1ha!ha! kuna vitu vingi nimefunika funika ila ndo hivyo km ulikusudiwa utanilewa mnoo..........
mbarikiwe