Ads 468x60px

Thursday, April 21, 2016

NYUMA YA PAZIA.................

Eeh bwana situkafanya boat cruise...... lengo kwenda tuu kuona wenzetu wanavyoishi.............  mi na Baba watoto wangu tumekutana yeye anapenda mnoo kucheza majini, yaani kunamichezo anachezaga mimi pembeni nahisi roho inatoka ha!ha!ha! lakini mi mkewe napenda view ya maji aisee ........ yaani ukinipeleka mafichoni  km ni eneo la maji maji naomba chumba kinachotazamana na  maji yaani kwa garama yoyote ntajitutumua (iwe ndani ya uwezo wangu lakini ha!ha!ha!) ila kuingia kwenye maji sasa ki!ki!kiii!

 Basi bwana tukafunga safari huko yaani nyumba zimejengwa  back yard mtu kapaki boat lake duuu!! we unafunga safari kwenda kuangalia dolfin mwenzio ndo nje kwake anapumzika ha!ha!ha!  tunajifungaga safari humu ndani kwenda fishing wenzetu wanafish nje ya nyumba ....... Duuu!!! ila kiukweli huku mafichoni ninakoendaga aisee kunanipaga mtazamo tofauti aisee..........

 na hii nimejikuta sina hela ila ndoto zangu zinakuwaga kubwa mpaka naogopa na pia imetusaidia sana kuona vitu kawaidaaa....... nakutokuwa na haraka zaidi kujipanga.... Yes inawezekana mbona nilivyokuwa umri fulani niliwahi kuaminishwa hapa nilipo  ningeweza kuona kwenye Tv pekee yake yaani ni ndoto kuwa !!! leo najiona ni zaidi ya ile ndoto basi na haya mengine yatawezekana Mungu atupe uzima nakuzidi kutuangazia neema yake.....


It is possible with Christ.........

nani hawaNdoto! andika ndoto yako.........
 Hapo Dolfin alipita ndo kumshangaaje sasa Ha!ha!ha!

 Yes  hii ndio ninayoizungumzia, Hizo nyumba za watu tuu kama mimi na wewe, tena nikuambiaje nilivyokuwa napewa historia niliambiwa wengi niwale walioretire ndo wamekuja na hela zako Bwana wewe why wait  mpaka huko kote????? Why why why...........


Tulivyokuwa wabishi mbona tuliwasiliana na wauzaji  ha!ha!ha! Mambo mengine yanatisha tuu kwa picha ila yanawezekana afanye akili yako iwaze tofauti............... na utakuwa tofauti

 Memory 


Tunawapenda

5 comments:

 1. Wazungu wanasema "if you believe it you can archive it"....... Maficho mema na mjienjoy!!

  ReplyDelete
 2. Mmenogajeeee!!! mweeh vinawezekana kweli??

  ReplyDelete
 3. mama wawili jamani nimekumic huku uje hata ukifanya kwa wiki mbili once sio mbaya, pulizzzzzzzzzzzzzzzzzz.

  ReplyDelete
 4. rose uko wapiii

  ReplyDelete
  Replies
  1. Sijatekwa mpenzi nipo njoo Instagram Wangu @rose wa Mbeyela

   Delete